Ugunduzi uliofanywa na Israel unaweza kutatua dhana ya muda mrefu ya kwenye biblia kuhusu asili ya wafilisti.
Timu ya wanaakiolojia wanachimba makaburi ya kale ya wafilisti karibu na eneo la Ashkelon, Israel. Wataalamu hao wa mambo ya kale wametangaza kua wamefanikiwa kwa mara ya kwanza kugundua makaburi ya wafilisti ambayo hayajawahi kugunduliwa hapo kabla. Kwa sasa wanaakiolojia hao wanafanya vipimo vya DNA, Miale ya ukaa na vipimo vingine kwenye mifupa ya watu hao inayokadiriwa kua ni ya kati ya karne ya 11 hadi ya 8 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo.
"Baada ya miongo kadhaa ya kutafiti mabaki ya vitu vilivyoachwa na wafilisti, hatimaye sasa tumekutana na watu wenyewe," Alisema Daniel M. Master, profesa wa akiolojia kutoka chuo cha Wheaton. Kutokana na utafiti huu wataalamu hao wanaweza kufumbua fumbo la mda mrefu juu ya asili ya watu hao.
Wafilisti walikua ni wageni kutoka magharibi na wanahusishwa na maeneo ya Ugiriki, Crete au Cyprus na wengne wanadai ni Anatolia-Uturuki, na maeneo mbali mbali ya ulaya japo haijulikani ni eneo gani hasa walitoka. Licha ya kua utafiti huu ulifanyika mwaka 2013 lakini matokeo yake wametangazwa mwaka huu kwani walihofia maandamano ya waisraeli wahafidhina wanaopinga kufukuliwa kwa makaburi hayo kwa kua wafilisti walikua ni adui mkubwa wa Israel na mmoja wao alikua ni Goliath ambaye aliuawa na Daudi kabla ya kua mfalme wa Israel. Hata hivyo wanaakiolojia hawa waliona vitu vya thamani na silaha japo kwa muonekano wa mwanzo haioneshi moja kwa moja kama watu hawa walikua wagomvi au wabaya.
No comments:
Post a Comment