Friday, 15 July 2016

JUVENTUS WAMNASA GONZALO HIGUAIN

Juventus wafikia makubaliano na mpachika mabao wa Napoli, Higuain.
Mabingwa wa Italia wamefanya makubaliano ya mkataba wa miaka minne na kiungo wa Napoli Gonzalo Higuain wenye thamani ya Euro milioni saba(€7milion) kwa msimu kwa mujibu wa mtandao wa goal.com.


Higuain alikua akihusishwa na vilabu kadhaa ikiwamo Arsenal ya England baada ya kufunga magoli 36 kati ya michezo 35 aliyoichezea Napoli. Hata hivyo juventus wanakataa dau la €94 milion wakitaka kutoa mchezaji wao mmoja pamoja na pesa ili kumnasa Higuain. Miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuhusika na mabadiloshano hayo ni Roberto Pereyra au Daniele Rugani.
Mkurugenzi mkuu wa Juventus Giuseppe Morotta atakutana na maafisa wa Napoli ili kukamilisha dili hili kwa siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment