Imekua sio kawaida hata kidogo kwa aliyekua kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kuzungumziwa kwa upande hasi kwani kila mwafrika ukiacha wachache sana walikua na bado wanaamini Gaddafi alikua ni mpiganaji wa bara la Afrika.
Itakumbukwa mchango wa Gaddafi kwenye umoja wa Afrika(Au) lakini pia mchango wake kwenye umoja wa mataifa. Hili lilikua ni jambo lililokua linampa Gaddafi umaarufu. Pia aliweza kuwakosoa watu wa magharibi bila uoga. Lakini hivi karibuni kumezuka kile kinachosemwa kama upande wa pili wa Gaddafi ambapo kwa mujibu wa taarifa hizi zinadai kua Gaddafi alitaka kua "Mfalme wa Afrika; Mfalme wa Wafalme" ambapo kila kiongozi wa Afrika na kila taifa la Afrika lingekua chini yake. Alitaka kutengeneza sarafu yake yenye nguvu zaidi ambapo kama ingefanikiwa basi Libya pia lingekua ni taifa lenye nguvu japo hii pia ingeinua uchumi mzima wa bara la Afrika. Na taarifa hizi zinadai sio mara moja au mbili, Gaddafi amewaita viongozi wenzake wa Afrika "Watumwa".
Na shahidi mbali mbali zimetolewa japo zimeonekana kwenye mitandao michache kwa hio usahihi au ukweli wake bado ni kitu cha kutiliwa shaka.
(Usisahau kuweka mtazamo wako juu ya hili)
Kwa maelezo zaidi juu ya taarifa hii soma hapa……>>>http://trendingmedias.com/the-truth-about-gaddafi-he-was-no-friend-of-africans-he-only-wanted-to-rule-them
No comments:
Post a Comment