Tuesday, 12 July 2016

SMARTWATCH YAKO INAWEZA KUWAPA WAHALIFU NAMBA YAKO YA SIRI YA ATM.

Smartwatch na vifaa vingne tunavyovivaa mwilini vinaweza kutoa namba yako ya siri ya ATM kwa wadukuzi "hackers".


Utafiti mpya uliofanywa na wataalamu kutoka chuo kikuu cha Binghamton umeeleza kua vifaa tunavyo vivaa mwilini (wearable devices) kama vile saa za kidigitali (smartwatch) vinaweza visiwe salama kabisa kama tunavyofikiria kwani vinaweza kuvujisha namba yako ya siri ya ATM.

Kutokana na watafiti hao hatari inakuja kwenye "motion sensors" (vihisishi vya mwendo) ambavyo vimewekwa kwenye vifaa kama smartwach.
Licha ya sensor hizi kurekodi taarifa zingne pia hurekodi mwenendo wa mkono wako kitu ambacho kinaweza kuwapa mwanya wadukuzi kuweza kutoa uelekeo wa mkono wa mtumiaji na kutoa taarifa za nini mkono ulikua umefanya. Watafiti hao walifanya majaribio mbali mbali na kugundua kua ni kweli sensor hizo zinaweza kutoa taarifa hizo za ATM kwa wastani wa usahihi wa 80%!

Watafiti hao walibainisha kua wadukuzi hao wanaweza kutumia Bluetooth au program nyinginezo ambazo zitaiunganisha smartwatch yako na smartphone yako na wao kuweza kupata taarifa zako. Hivo watumiaji wa smartwatch wanashauriwa kutumia mkono ambao hauna wearable device yoyote wanapotumia ATM machine.

Tafadhari usisahau kuwashirikisha wenzako ujumbe huu.

No comments:

Post a Comment