Thursday, 14 July 2016

MAONI KUHUSU WALIMU KUKATWA MSHAHARA JUU YA MADAWATI

WALIMU KUKATWA MISHAHARA KWA SHULE AMBAZO WANAFUNZI WATAVUNJA MADAWATI.

Nikifuatilia kauli za serikali kwa mwaka 2016 sishangai saana kuona kauli hii ikitoka. Inaumiza saana kwa wenye taaluma ya ualimu lakini licha ya mchango mkubwa wa mwalimu kumbukeni huko nje jamii ndo inavowachukulia. Yaani mwalimu unaweza kusemwa kwa vyovyote vile na watu wengi wakaona sawa.


Binafsi nmehuzunika,nmeumia na kauli ya Mh.Raisi wetu kua mwalimu akatwe mshahara kwa madawati yatayovunjwa na mwanafunzi. Najiuliza hivi katika nchi hii ni watumishi wangapi "wateja" wao wamevurunda na wakawajibika?? Hivi labda mnisaidie tuu..halmashauri gani imevurunda aaf viongozi wa halmashauri wakakatwa mishahara? Kwa hio na taifa kama hatufiki tunatakiwa kufika........nduki!!

Aafu kitu kimoja labda watu hawakielewi. Mwalimu client/mteja wake mkuu ni "mtoto"(6-18yrs) hawa ndo wateja wa mwalimu. Wana michezo mingi, mambo mengi!! Lakini kwa kosa la mtoto mwalimu abebe mzigo daah!! Huyu mwalimu atakua na kazi ya kuangalia wanafunzi wanaovunja madawati pekee? Najua hana kazi nyingi kama wengine hizi ni baadhi tu.
√Kuangalia maendeleo ya KILA mwanafunzi katika taaluma,afya, usafi n.k
√Kuandaa kujaza mipango kazi ya masomo yake.(apo kumbuka ana masomo zaidi ya mawili)
√Kuandaa mitihani ya ndani na nje ya shule.
√Kusimamia nidham ya watoto(maadili kwa upana wake na kwa wingi wa wanafunzi)
√Kazi za kiutawala kama kuandaa baadhi ya ripoti.
√Kuandaa notes za madarasa yote(achana na kufundisha kwanza....kumbuka inabidii usome zaid ya vitabu vitatu hvi ili notes ziwe bora.)
√Huyo mwalimu bado anapaswa kuhakikisha watoto wanacheza, mazingira safi....miradi ya shule daah
√Ana vipindi zaid ya 24 kwa wiki na lazima afundishe vyote.
√Inatakiwa atoe mazoezi na majaribio na kusahihisha mazoezi yote. Na kumuelekeza kila mwanafunzi makosa yake.
Daah bado huko mtaani ana majukumu mengine ya kijamii.

Jamani hizi ni baadhi tuu...kwa hio kwa sasa na kulinda madawati duuuh!! Okay Naamini mwalimu ndiye mtengenezaji wa wataalam wengne. Asa sio vibaya hata tukiweka "heshima ya kitaaluma" japo kwa udogo wake inatosha. Kumbuka tangu ukiwa na miaka 7(ulipoanza shule) umetumia mda mrefu zaidi ukiwa na mwalimu kuliko hata mzazi wako!!!

____"Najivunia ualimu wangu na siionei haya taaluma yangu"___

            ©Big Oppa

No comments:

Post a Comment