Sunday, 10 July 2016

MWALIMU MKUU HUYU ANATUFAA SISI? (Sehemu ya 2)

HEADMASTER/MWALIMU MKUU
SEHEMU YA PILI.
Inaendelea ilipoiashia...


Namkumbuka mwalimu huyu wa tatu hakukaa sana. Alikaa kipindi sawa na Mr. FreweAir. Lakini alichokifanya alituletea mifumo mipya na kuiendeza ile ya mwalimu FreeAir. Alitusisitiza kutokufunga madirisha ila asema tujihadhari na "nzi". Shule yetu ilikua na mali nyingi lakini alisema shule haina uwezo wa kuzisimamia hivyo akaamua kuziuza, kinachoniuma ni kwamba aliziuza kwa "bei chee". Somo kuu alilolihubiri kila siku ilikua ni "utandawizi". Alihubiri utandawizi kama injili. Kutokana na kua lilikua ni somo jipya watu walikata tamaa kwani walikua hawaelewi. Wageni wengi waliletwa shuleni kila mgeni alikua na mkoba wake, camera, kidaftari kidogo na kalamu. Walichora kila kitu cha shule kwenye vile vitabu vidogo wakampa mwalimu mkuu wetu atie sahihi kama "ukumbusho". Tulijaribu kuhoji kuhusu michoro hiyo ila tulipigwa na kufukuzwa shule.

Haikua rahisi saana kuishi kwa raha ukiwa muulizaji mzuri wa maswali. Lakini kwa kua wale wageni walikua wakija na "vijizawadi" na kugawa kwa baadhi ya wanafunzi, walimu na kamati ya shule ilionekana kama maisha yameboreshwa zaidi kipindi cha mwalimu Global kuliko kile cha FreeAir. Hata wageni wanafiki walimsifia na kuisifia shule kwa kusema eti imeanza kuimarika! Ni usemi wa kipumbavu kwani wanafunzi tulikua na njaa, hatukua na sare, maji, wala madaftari, hatukua vyumba vya darasa, madawati wala chaki. Hatukua na maktaba wa maabara. Hatukua na chochote isipokua miili iliyodhoofu kwa kukosa mahitaji. Ningali bado nakumbuka maumivu ya kwenda shule bila viatu na baridi kali ya mkoani Njombe. Ningali naikumbuka kauli ya mwalimu mmoja kua ni bora niende peku shule, nile majani au mchanga lakini eti shule haiwezi "kumpigisha kwata" mwalimu mkuu kwani alikua mtu wa miraba minne. Nikajiuliza kwa hiyo mwalimu mzuri ni yule anayejali maslahi yake au yule anaejali maslahi ya wanafunzi walio wengi ambao ndio walimu wa kesho?? Mipango mingi hewa, taasisi hewa vilianzishwa ili kupumbaza akili za wazazi na wanafunzi. Mipango hiyo ilipewa jina la kupunguza umaskini. Lakini maskini kumbe mpango wenyewe uliletwa na wageni wale wanafiki na wazandiki wanye hila na shule yetu. Walipotoa "vijizawadi vidogo" wao walipewa zawadi kubwa kwenye bahashasha na zingine walifungashiwa kwenye yale mabegi yao yalokuja matupu. Si haba tufikia ukomo na mwalimu global.

Kulikua na tumaini miongoni mwetu kua sio muda maisha yangebadilika. Nyuso za furaha na tabasamu zilikua zinaongezeka mtaani. Hatimae tulimpata mwalimu mkuu mpya. Akiwa mtu wa watu, mcheshi na mpole. Mpole kweli hadi maamuzi yalikua ya kipole. Alikua ni nyota njema kwa wanafunzi na wazazi.Lakini ghafla alijawa na kiburi na dharau baada ya kuona "kama anaweza". Aliendeleza mifumo mingi ilokuepo awali. Akitupilia mbali ushauri wa wakongwe na kufuata njia zake.

Nakumbuka siku moja mvua kubwa iliambatana na upepo iliikumba shule yetu. Mapaa yakaezuliwa, kuta zikateneza nyufa, madirisha yalipasuka na milango kung'oka. Wote tukajikuta tunatazama hatuna la kufanya. Mkuu wa shule alitetemeka sana lakini ilikua ishatokea. Wengi wakajua udhaifu wa shule yetu na hapo hapo mengi yakaonekana. Tulikaa chini kwenye udongo kwa kukosa madawati, tulikua wachafu kwa vumbi la darasa, hatukua na ubao wala chaki. Alihubiri kuomba misaada ili kuikarabati shule lakini hakuwahi "kujitutumua" kutafuta pesa zake ili tukarabati shule. Tuliendelea kulia njaa, tulipigwa na upepo na vumbi kipindi cha jua tukaungua na kipindi cha baridi tukatetemeka na kuungua midomo, kipindi cha mvua tulilowa chapachapa. Tulipiga kelele tukimtaka aangalie upya anachokifanya lakini alitabasamu na kusema "hata mimi sijui nafanya nini ila tunaweza kuendelea hakuna shida".

Kutokana na kushindwa kabisa kuendeleza ile furaha ya wanafunzi alijikuta akikosolewa sana lakini hakujali. Vitu vya kifahari vilimiminika kwenye ofisi ya walimu na kamati ya shule lakini hata kidogo havikwenda kwa mwanafunzi. Shule ikawa ya ovyo saana hakuna anaejali!! Mwalimu mkuu hajali, mwalimu hajali, wajumbe wa kamati ya shule hawajali na mwanafunzi akajikuta anafundishwa kutojali. Maana alipolia hakuna aloskia kilio chake na alipocheka hakuna alotambua kicheko chake. Akatambua kumbe hakuna anaejali, kwanini mimi nijali??/

Mwanafunzi hakuthaminiwa waliojitolea kua viranja wa shule walipigwa na kuumizwa na kufukuzwa shule. Shule ikapitiliza ukatili na ujeuli, hatukufundishwa ila tulijifundisha...!
Baadae nilimskia mwalimu mkuu akisema amechoka kua mwalimu mkuu anataka kupumzika..kila mwanafunzi alifurahi kwa kua aliamini atasoma kwenye shule alokua akiiota!!

(Itaendelea....)

No comments:

Post a Comment