Monday, 11 July 2016

URENO WATWAA UBINGWA WA EURO 2016 BILA CHRISTIANO RONALDO

Hatimaye timu ya taifa ya Ureno imetwaa kombe la mataifa ya Ulaya (EURO)2016 baadaya kuwazaba wenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ufaransa goli 1-0.
Tofauti na matarajio ya wengi kua huenda labda timu ya taifa ya ufaransa ingetwaa kombe hilo kutokana na kikosi hicho kusheheni wachezaji nyota na pia kucheza kwenye ardhi yao ya nyumbani lakini ilikua ni Ureno timu ambayo ilianza kwa kusuasua katika mashindano haya.

Ureno wameshinda bila kuwepo kwa mshambuliaji wao machachari na kapteni wa timu hio Christiano Ronaldo ambaye alipata majeraha ya goti baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa pembeni wa ufaransa Dimitri Payet mwanzo mwa mchezo huo uliokua unapigwa kwenye dimba la Estade de France. Hata hivyo alikua ni mshambuliaji wa Lile, Éderzito António Macedo Lopes anayefahamika kwa jina la Eder aliyewashindia Ureno mnamo dakika ya 109 ikiwa zimebaki dakika 11 tu mchezo kumalizika.

No comments:

Post a Comment