Ujerumani sasa inayatambua mauaji ya watu wa jamii ya waherero kama mauaji ya halaiki.
Serikali ya ujerumani mjini Berlin sasa imeyatambua rasmi mauaji yaliyofanywa na nchi hiyo kipindi cha ukoloni katika koloni la ujerumani ya kusini-Magharibi ambayo ni Namibia ya sasa kama yalikua ni mauaji ya halaiki.
Kati ya mwaka 1904 na 1908 wanajeshi wa kijerumani waliwaua takribani watu 100,000 wa jamii ya wa-Herero na wa-Nama huko Namibia. Kufuatia vuguvugu lilioanza mwaka 1904, Jenerali Lothat Von Trotha aliamuru kuangamizwa kwa jamii hiyo.
Kwa muda mrefu kumekua na mvutano ndani ya Bundestag (bunge la ujerumani) kama mauaji hayo yaingizwe kwenye orodha ya mauaji ya halaiki au la. Hata hivyo ujerumani inasema kua hakuna madhara yoyote yale ambayo itayapata kwa kuyatambua mauaji hayo kama mauaji ya halaiki. Ikumbukwe kua mapema mwaka huu Ujerumani iliyatambua mauaji ya Waarmenia kama mauaji ya halaiki. Hata hivyo waraka uliotolewa na serikali unaeleza kua mazungumzo baina ya serikali ya Ujerumani na Namibia hayalengi katika ulipaji fidia kwa wahanga wa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment