MNYIKA; SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA.

Dar es Salaam. Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekanusha taarifa zinazodai kuwa anataka kuachana na chama hicho.

 Mnyika amesema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba amesisitiza kwamba huo ni uzushi.
“Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama,” amesema.
Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.
Uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa katibu mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.


Source: Gazeti Mwananchi

Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?