Wednesday, 13 July 2016

UKWELI UNAUMIZA ILA UONGO UNAUA!

UKWELI UNAUMA NA KUUMIZA ILA UONGO NDIO UNAOUA.

Uoga ni zao la Uongo. Na ni mwaanzo wa kufilisika kiutu na ni angamizo la mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Hakuna sababu ya kuzuia imani yako kwa woga wako. Unachokiamini kutoka moyoni ni bora kuliko unachokionesha machoni au kukisema mdomoni.(Uoga ni kua unajiongopea hadi mwenyewe; Umekua muongo mpka unapokosa wa kumdamganya basi unajidanganya mwenyewe).


Kwa mda mrefu wengi tumekua wanafiki kwa uoga uliondani yetu na kutokana na uoga tumekuza unafiki na anguko la jamii. Leo hii mwanafunzi ni mwoga, mkulima ni mwoga, wanasiasa waoga, raia waoga...kila mtu ni muoga na kila mtu kawa "mnafiki kiaina" japo kuna wachache wanajinasua kwenye unafiki huu.

Kwa taaluma yangu ndogo lakini muhimu nimejifunza uoga huu tumepandikizwa kwa kutaka sifa za kijinga. Leo elimu yetu haipimi uelewa ila inapima ufaulu kwa mfumo wataalamu wanauita "Learning for test". Watoto wakariri past paper wapate sifa za kufaulu. Huu ni upuuzi.(Dhana ya elimu iwe kwaajili ya kupima uelewa kwamba hata baada au nje ya shule unaweza kuleta mabadiliko). Wamefaulu mtihani shule wamefeli maishani.

Leo wanasiasa wanaongea "kinafiki" ili mradi tu wapate kutambulika (recognition) na sifa ambazo sio zao haswa! Wamepika ripoti zikapigiwa makofi, sijui sijui mara hati safi...kumbe madudu mtupu!

Leo hii watu wanashindwa kufanya maamuzi sahihi kisa wamejawa na uoga...ukisikiliza kauli za viongozi wetu leo mpaka unaogopa kwamba kaizungumza kwa shinikizo au kapitiwa? Yote hii ni uoga umetawala. Naamini na ninaelewa wananchi wengi tuna utashi mdogo wa kisiasa ila tunapoelekea kama hatutafuti ukweli basi tumeamua kujitoa sadaka. Uhalalishwaji wa vitu vidogo vidogo gharama zake ni kubwa ndugu zangu. Chukulia mfano wa mauaji ya polisi watano kule Dallas, Marekani. Swala hili halijaanza juzi ni la mda mrefu ila ni ile watu wanachukulia poa poa. Mimi naamini sisi watanzania, sisi waafrika tunaweza kuiepuka hatari inayotukabili kwa kua wakweli. Ukweli ni silaha ya kuangamiza UJINGA, UMASKINI, UTUMWĂ€ NA UNAFIKI.

Ila kuupata ukweli sio kazi ndogo ndugu zangu. Mwanahistoria Edward H. Carr aliwahi kusema hivi(Ni tafsri isiyo rasmi tafadhari);
"Ukweli hasa sio sawa na samaki ndani ya mtego wa mvuvi. Ni sawa na samaki wanaoogelea kwenye bahari kubwa na wakati flani kwenye eneo ambalo halifikiki; na kile mwanahistoria anachokipata kitategemea kwa kiasi flani bahati, na kwa kiwango kikubwa itategemea ni upande gani wa bahari amaeamua kuvua na njia anayoamua kuitumia. Mambo hayo mawili yatategemeana na aina ya samaki anaotaka kuwavua."

Kwa hio ukweli upo mahali umejificha na ili kuupata lazma utumie mbinu mbalimbali. Swali langu kwako ni je unautafuta ukweli au utaendelea kua mnafiki?
Kwenye biblia kuna mistari inasema "Kweli itakuweka huru". Kwa maana hii kama huujui ukweli wewe hauko huru; NI MTUMWA! Kwa maneno ya hayati mwalimu Nyerere ni "bora mtu akutumishe mwili na sio akili"
 Utumwa wa kiakili ni MBAYA KULIKO. Na kama akili yako imetekwa jua huendi popote! Utazungushwa sehemu moja kama mdori wa upepo. Watakufanya kila baya watakakalo kwa kua wamekushika akili yako, huwezi tena kufikiri mwenyewe mpka wakufirishe wanachotaka! C'omon guys!! Huu muda ni muda wa kufikiri kwa akili yako ukiwa huru na sio mtu aitumikishe akili yako. Swali la pili utakua mtumwa mpka lini??

Kila kitu kina mipaka yake uongo mpka wake ni ukweli, maji ni nchi kavu, mchana ni usiku, ardhi ni anga...kila kitu kina mpaka. Hata mateso pia yanampaka!! Kuonewa? Kunyanyaswa? Hakuna kitu kitakacho dumu milele. Leo hii unatafuta sifa za kila aina ila siku ukiwa ICU juu ya kitanda cha wagonjwa utaamini kua sauti za wanyonge zilizopiga kelele huku wewe ukiwa busy kutafuta sifa na utajiri zinakuumiza kuliko hata ugonjwa ulonao. Tukiamua kuwafanya watu weng kua na furaha, niamini mimi, ile furaha yao ni faraja yako kubwa siku ukiwa ICU juu ya kitanda cha wagonjwa na licha ya ugonjwa utakuta unatabasamu.

"UKWELI UTAKUWEKA HURU". USIOGOPE KUUTAFUTA POPOTE UTAKAPO PATIKANA.

Ukitaka kusoma jumbe nyingine kama hizi ziko nyingi tu
 Tembelea: www.kielelezo.blogspot.com

No comments:

Post a Comment