Monday, 11 July 2016

UEFA YAMTAJA MCHEZAJI BORA WA EURO 2016

Leo jumatatu UEFA imemtaja mshambuliaji wa ufaransa na mfungaji bora wa mashindano hayo Antoine Griezmann kua ndiye mchezaji bora ya michuano ya ulaya kwa mwaka 2016.

"Antoine Griezmann alikua ni hatari kwenye kila mchezo aliocheza. Amefanya kazi kubwa kwa timu yake na ana ujuzi, maono na umaliziaji mzuri", alisema mkurugenzi wa benchi la ufundi la UEFA Ioan Luspescu, aliyeongoza wataalam waliomchagua mchezaji huyo.

Sir Alex Ferguson, meneja wa zamani wa klabu ya Manchester United alikua miongoni mwa watu 13 waliokua wakitazama kwa karibu mchezo huo. Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 25 ,ambaye kwa kupoteza mchezo wa jumapili dhidi ya ureno inamfanya kupoteza fainali mbili ndani ya miezi miwili kwani hapo kabla alipoteza fainali ya champions league dhidi ya mahasimu wao Real Madrid. Lakini pia Griezmann alishinda kiatu cha dhahabu baada ya kufunga magoli sita kwenye mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment