Tuesday, 5 July 2016

FBI WATOA TAARIFA YAO YA UCHUNGUZI DHIDI YA HILLARY CLINTON

HILLARY CLINTON KAKALIA KUTI KAVU??

FBI wametoa taarifa yao ya uchunguzi juu ya tuhuma zinazo mkabili mgombea wa wa uraisi wa marekani kupitia chama cha Democrat,
Hillary Clinton. Bi Clinton anashutumiwa kutumia barua pepe binafsi kutoa siri za nchi hiyo wakati alipokua waziri wa mambo ya nchi. Katika taarifa uliyotolewa na mkurungenzi wa FBI James comey imeweka baadhi ya mambo na kusema kua wao hawana shida na maamuzi yatakayotolewa na mahakama kuu ya nchi hiyo kwa kua kazi yao ilikua ni kuchunguza kazi ambayo wameimaliza. Mambo yaliyotolewa na FBI kati ya mengine ni pamoja na;
>Kati ya email 30,000 kuna email kadhaa ni za siri ya kujuu(top secret) zingne zimewekwa kama ni "classified" na nyingne za siri ya chini zimewekwa kama "confidential".
>Hakuna "Archives" (meseji zilizosalia/kumbukumbu) kwenye barua pepe ya waziri wa mambo ya nje Hilary Clinton.
> Hillary na Wanasheria huenda walizifuta baadhi ya barua pepe.
>FBI ilikua kama inaunganisha vipande vya ushahidi.
>Kulikua na uzembe mkubwa mno juu ya kuzitunza na kuhudumia siri za taifa la marekani.
>Hakukua na ulinzi wa muda wote juu ya barua pepe hizo kama ilivyo kwa taarifa zingne za ofisi hio na taasisi nyingne za marekani.
>Kutokuwepo kwa neno linaloonesha kua hiyo taarifa ni "classified" hakuondoi ukweli kua taarifa hio ilichukuliwa ndivyo sivyo.
> Kama barua pepe ya Hillary ilidukuliwa inakua ni ngumu kutambua hilo.
>Kulikua na kiwango kidogo cha ulinzi wa taarifa za wizara hio kwa kipindi hicho.

No comments:

Post a Comment