Tuesday, 5 July 2016

DONALD TRUMP NA MAREKAMI MPYA.

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya Marekani.

1. Wamarekami wengi wenye asili ya kiarabu walishangilia lile shambulizi la september 11 2001. Hili ni shambulio baya kabisa kwa nchi ya marekani miongo kadhaa.

2. Anaamin kua miskiti yote nchin marekani inapaswa
kuchunguzwa na waislamu wote wafuatiliwe kwa ukaribu kabisa kwa kutumia kitengo cha kupambana na ugaidi.

3 Njia za "waterboarding" na.nyingne njia ngumu ndo zitumike kwenye kuwahoji magaidi. (waterboarding ni njia ya mateso inayotumiwa na mashorika ya kijasusi kama CIA) unateswa kwa kutumia maji ukiwa kichwa chini.

4. Trump pekee anaeweza kualiangamiza kundi la IS. Haoni mgombea mwingne mwenye huo uwezo.

5. Kuweka "code" mpya kwenye kodi. Anasema atasamehe kodi kwa wenye kipato chini ya $25,000 na atapunguza kodi hadi kufikia 15% kwa wafanyabiashara wakubwa na kuruhusu makampuni makubwa kuweka pesa zao nje.

6. Kujenga ukuta mkubwa kabisa kati ya marekani na mexico. yeye anaona wamexico n wauza madawa na wabakaji. Ukuta huo unaweza kugharimu hadi $13bil!!

7.Kuwarudisha makwao zaid ya wakimbizi 11 milioni. Licha ya gharama lakin anasema mpango huu unawezeka. BBC walikadiria mpango huu unaeza kugharimu zaidi ya $144milion

8.Putin anaweza kukaa kwenye mstari. Anaamini Obama na Putin wanachukuliana kama maadui. Lakini yeye anaamini kua anauwezo wa kufanya mazungumzo na URUSI.

9. Ili kupunguza mauaji ya kiholela lazima Marekani iwekeze katika matibabu ya matatizo ya akili "mental treatment". Yeye haoni kama kufanyiwa marekebisho sheria ya udhibiti wa umiliki wa silaha kama ni suluhisho la kudumu.


10. Marekani lazima "ile sahani moja" na China. anaamini china inashusha thamani ya pesa yake ili iweze kuuza nje. Hili atalipinga na kuitaka China ifuate viwango vya kimataifa vya ubora wa mazingira na wafanyakazi wake.

(Itaendelea......)

No comments:

Post a Comment