Raisi wa marekani Barack Obama amefanya kampeni na aliyekua waziri wa mambo ya nje
Hillary Clinton katika kuhakikisha mgombea huyo wa kiti cha uraisi kupitia Democrat anashinda katika mbio zake za kua raisi wa taifa hilo lenye nguvu zaidi duniani. Raisi Obama anaamini kua Hillary Clinton atashinda uchaguzi wa mwakani kutokana na sera zake.
Raisi Obama alikonga nyoyo za mashabiki wengi waliohudhuria mkutano wa kampeni za Hillary Clinton huko Charlotte, North Carolina siku ya jumanne. Akimuelezea waziri huyo wa zamani Obama alisema Hillary Clinton ni mtu mwenye uelewa mkubwa, mwenye uwezo mkubwa, anafanya kazi kwa bidii, mwenye maamuzi magumu na mtu anaependa kazi yake.
Katika hatua nyingine Hillary Clinton anakosolewa vikali na baadhi ya wamarekani hasa kutoka upande wa Republican kwani kutokana na uchunguzi wa FBI wanaamini Hillary ni muongo na uongo huo unahatarisha taifa la marekani.
No comments:
Post a Comment