Ulishawahi kukaa ukafikiria kama unahitaji kufuta taarifa zako kutoka Google? Sasa usiwaze kila kitu ni kirahisi. Labda ulishawahi kutumia Google kutafuta taarifa flani na
hutaki ile kumbukumbu ibaki Google. Siku hizi Google wanekurahisishia maisha unaweza kufuta hatua chache tu na ukamaliza kazi.
Ukweli ni kwamba google wamehifadhi taarifa zako nyingi sana. Mfano mmbo unayoyatafuta mara kwa mara, namna na muda wa kuperuzi, kurasa unazoperuzi (ukiwa umeingia kwenye akaunti ya google kwa kutumia "browsers" zilizoko kwenye kifaa chako).
Kuna watu hawataki taarifa zao zibaki Google na wanataka kuzifuta na Google wanakuruhusu kufuta taarifa zako kwa kufanya yafuatayo.
1. Kama ni mjanja kuna mfumo huitwa "Incognito". Ukiweka ON taarifa zako hazihifadhiwi! Ipo kwa baadhi ya browers kama vile Uc browser.
2. Ukiwa ushatumia bila "Incognito" unaweza kufuta kwa kusafisha au kufuta historia na cookies. (Clear serch history >> clear cookies) taarifa zako zinafutika kwenye akaunti ya Google kwenye kifaa chako ila ukitumia kifaa kingine bado utaziona.
3. Computer ingia kwenye account yako ya Google >> history.google.com
Hapo utakutana na taarifa zako na utachagua unayotaka kufuta na kisha bonyeza kitufe kilichopo upande wako wa kusho kimeandikwa REMOVE.
Au simu
Ingia kwenye akaunti yako ya Google >> settings >> history (utaona taarifa zako)>> manage. Chini yake kuna kitufe kimeandikwa REMOVE utachagua taarifa unayotaka kuiondoa kisha utabonyeza REMOVE.
AU
Kwenye pembe ya kulia juu kuna alama pale ibonyeze itakupa machagua ya kufuta aina za taarifa, na muda muda kwa pamoja.
Nadhani sasa unaweza kifurahiaaisha. Comment yako hapo chini tafadhari.
No comments:
Post a Comment