Thursday, 7 July 2016
MANISPAA YA IRINGA YANG'ARA NG'ARING'ARI
Manispaa ya iringa imeibuka idedea kwenye swala la usafi kitaifa. Manispaa hio imeipiku manispaa ya moshi ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikiongoza kwa usafi.
Ushindi huo wa manispaa ya iringa unakuja ambapo taifa zima kwa sasa lipo kwenye kampeni kubwa ya usafi kitaifa ambayo ilianza rasmi mwishoni mwa mwaka 2015.
Akizungumza na Ebony fm kwenye jicho pembuzi mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Alex Kimbe ameelezea jitihada zinazofanywa na uongozi wa manispaa hio ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya usafi na kufanya matangazo pale siku ya usafi inapokaribia lakini pia amepongeza wananchi wa manispaa hio kwa kua wasikivu na waelewa kwani wamemekuwa wakisaidiana vizuri na manispaa katika kuhakikisha swala la usafi linafanyika ipasavyo. Pia, mstahiki meya huyo amekipongeza kituo cha Ebony fm kwa mchango wake mkubwa kutangaza kampeni za usafi.
Lakini pia mstahiki meya huyo ameeleza kua wana mpango wa kupanda miti katika manispaa ya iringi. Mstahiki meya huyo amesema tayari kwa kushirikiana na watu wa maliasili wamekwisha kuotesha miti ambayo itagawiwa bure kwa wananchi hapo baadae ili kila kaya ipande angalau miti mitano ili kuiweka manispaa hio katika mandhari nzuri. Pia, miti hiyo itapandwa pembezoni mwa barabara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment