Usiidharau nguvu ya wajinga kwa maana wakiungana wana nguvu kubwa ya kuamua hata kama ni maamuzi ya kijinga.
Na pia wanasema usipende kubishana na mjinga kwani atatumia maarifa, ujuzi na uzoefu wake wa kijinga kukushinda wewe. Hata mimi pia nakubali madhara ya kubishana na mjinga yapo kwa mwenye akili na busara. Kumbuka wakati wewe unafikiria kumjibu kwa kujenga hoja, yeye anaropoka neno lolote ambalo litakua limejiokeza bila kuzingatia mambo mengne.
Lakini swala kubwa leo tuachane na hili la kubishana na mjinga bali tuangalie "Nguvu ya Mjinga". Kama mwanzo nilivosema mimi naamini mjinga ana nguvu na nguvu yake huonekana pale ambapo mtu huyu ataamua kutumia ujinga wake kufanya maamuzi. Hatuwezi kufika sehemu tukadharau nguvu ya wajinga. Hili kundi la watu katika jamii wakiungana wana ushawishi mkubwa na wanaweza kufanya chochote watakacho. Nilikua nafikiri kauli ya Plato aliposema "demokrasia ni utawala wa kishenzi" lakini mara nyingi niliona kama Plato aliteleza lakini baadae nikaja kujua kua ni kweli "demokrasia ni utawala wa kishenzi" kwa kua wajinga ni wengi katika jamii kwa hio kwa kuungana kwao mwisho wa siku wamefanya maamuzi ya kijinga ambayo yamegharimu maisha wenye akili na busara kutokana na uchache wao. Hatari inakuja pale wenye akili husindwa kuizuia hataro hii ambayo ni kubwa katika ustawi w jamii bora na endelevu. Ujinga ni hatari kwa ukuaji na ustawi wa maisha mtu(kiroho, kimwili na kiakili). Kama demokrasia ya kwenye makaratasi na kwenye majukwaa ingekua ndio hio inayotekelezwa basi demokrasia ingekua mfumo safi, kwa bahati mbaya sana "demokrasia ya darasani ni tofauti kabisa na demokrasia ya ofisini." Katika nchi ambayo inalitaja neno "demokrasia" eti watu wake ni waoga, hawana uhuru wa kujieleza na kutoa mawazo, wanapuuzwa, hawarusiwi kukosoa!! Unataka kuniambia chini ya jua kuna "Ideal government"? Hakuna serikali ilo thabiti na sahihi kwa asilimia mia moja kwenye kila hatua inayochukua. Haijalishi nini au nani ila "ilimradi jua linamulika basi jua huwezi kukikwepa kivuli". Kamwe huwezi kuzuia kivuli chako na huna sababu ya kukimbia kivuli chako, maana hutaweza.
Kwa hio nikitazama nchi 54 za Afrika nagundua "Tupo hapa tulipo kwa sababu ya nguvu ya wajinga". Tangu tulipojua kua wakiungana wanaweza ndio imekua pia ni pigo kwa wengine. Matatizo yetu ya vipindi vipindi ni matokeo ya "maamuzi ya kijinga kwenye chumba cha kupigia kura". Sio mbaya nadhani mjinga sio mwehu au mwendawazimu, mjinga akieleweshwa "vizuri" ataelewa.
Yaani wewe unaenda showroom unanunua bajaji alafu ukitoka nje unataka bajaji iwe kama Mercedes Benz! Hio ndoto haipo kabisa. Kwa hio tunapo mpa nyani kazi ya kulinda shamba mahindi au ndizi haitupasi kushangaa tutakapo kuta shamba halina kitu maana ujinga wetu utakua umetufikisha hapo. Kwa hio ni jukumu letu kama jamii kuhakikisha kua kwa gharama yoyote ile ujinga unapigwa vita ili basi vizazi vijavyo vijivumie sisi kuishi kabla yao. Kuendelea kuukumbatia ujinga ni dhambi na tutahukumiwa.
No comments:
Post a Comment