Saturday, 9 July 2016

FACEBOOK KUTUMIKA KUTUMA NA KUPOKEA PESA.

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni na hayawi hayawi sasa yamekua.


Kutokana na kile kinachoelezwa kua ni maendeleo ya sayansi na teknolojia kila siku watu wanabuni njia mpya za kuweza kuisadia jamii. Kwa sasa mmiliki wa mtandao wa Facebook, Mark Zukerburg ameendelea kua mbunifu kwa kuingiza programu ya kutuma na kupokea pesa kwa kutumia programu ya kutuma na kupokea ujumbe wa Facebook yaani "Facebook Messenger". Hivi karibuni wateja wa mtandao wa Facebook wanaotumia debit card inayotolewa na benki ya narekani wataweza kutuma na kupokea pesa kupitia mtao huo wa Facebook.

Unakumbuku mara ya kwanza kabisa wakati Facebook wameileta hii app ya messenger wengi walistuka na kuboreka kwanini upakue app kwaajili ya kuchati na rafiki wa Facebook pekee?? Lakini Mark alikua na lengo kubwa kuliko wengi tulivyofikiri. Alikua anataka kuwezesha kupiga simu za sauti na video, chess game na nani alijua kua malipo ya mtandaoni?? Ndio unaweza kutuma na kupokea pesa kupitia Facebook messenger kwa staili ya PayPal. Lakini ili kuweza kupata huduma hii lazima umiliki Debit card ambayo hutolewa na Benki Ya Marekani. Lakini huduma hii haitakua na gharama zozote zile lakini itakua na ulinzi mkubwa kulingana na Facebook wenyewe.

Ili kupata huda hii fanya hivi.

Hatua ya 1. Weka debit card yako kwenye Facebook messenger ili kutuma au kupokea pesa. Utabonyeza alama ya profile, shuka chini utakutana na "Payments" bonyeza "Add New Debit Card" kukamilisha hatua hio.

Hatua ya 2. Fungua kitufe cha kuchati na mtu unaetaka kumtumia pesa au mtu unaetaka kumuomba pesa. Bonyeza kitufe cha "more" kina vidoti vitatu kwenye kisanduku cha pembe nne.

Hatua ya 3. Bonyeza "Payments", kisha utaingia kwenye screen ya malipo kisha ingiza kiwango unachotaka kukituma kwa mtu huyo na ukumbuke kuweka ni malipo ya nini. Kisha bonyeza "Pay" utakua umemaliza.

Hatua ya 4. Ukitaka kuomba pesa kwa mfano. Bonyeza "Request" upande juu ya kioo chako, weka kiwango na sababu ya kuomba kisha bonyeza "Request" kukamilisha ombi lako. Na baada ya hapo utakua umemaliza kila kitu kupitia Facebook ni njia rahisi saana alafu ni buree. Huduma hii itaanza kutumika kwanza Marekani kabla ya kusambaa sehemu nyingine duniani.

No comments:

Post a Comment