Monday, 4 July 2016

NATO na Urusi "Kupooza" Mvutano.

NATO na Urusi kufanya mazungumzo ya pamoja baada ya kilele cha mazoezi ya kijeshi huko Warsaw.

NATO and Urusi watafanya mazungumzo rasmi mara  baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kijeshi mjini Warsaw wiki hii.

Muungano huo wa wanajeshi wa NATO unatarajia kujenga jeshi kubwa zaid kuwahi kutokea tangu kumalizika kwa vita baridi ikiwa ni hatua ya kujibu kile wanachokiona kama ni uchokozi wa taifa la Urusi kwa mataifa jirani hasa Ukraine.

Katibu wa mkuu NATO Gen Jens Stoltenberg alieleza kua Moscow ilikiteka kwa nguvu kipande cha Crimea kutoka Ukraini mwaka 2014. Pande hizo mbili zinakutana kwa mara ya kwanza tangu mwezi June 2014 ambapo mazungumzo yao yalitawaliwa na mivutano na kutokukubaliana baina yao juu ya swala lla Crimea.

Stolenberg aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kua baraza la "NATO-Russia" limekua na umuhimu mkubwa kwaajili ya kufanikisha majadiliano.
Mkutano huo unalenga kuzungumzia upunguzwaji wa hatari na uwazi ambapo mambo haya yamekuja baada ya kudunguliwa kwa ndege ya kijeshi ya Urusi mwezi Novemba mwaka jana katika mpaka wa Uturuki na Rusia na vile vile kufuatia hatua ya ndege ya kijeshi ya Urusi kupita karibu na ndege za kivita za Marekani.

Rusia imeishambulia NATO kwa mkakakati wake wa kijeshi   huku rais wa wa nchi hiyo Vladimir Putin akisema NATO wanachochea vita latika eneo la ulaya mashariki. NATO na Urusi wanatarajia kuanzisha mawasiliano ya karibu kabisa ili kuweza kuzuia na kuepuka hatari inayoweza kutokea baina ya mataifa hayo mawili hasimu na yenye ngubu duniani.
bik/kms (AFP, dpa)

No comments:

Post a Comment