Thursday, 7 July 2016

MESSI KUTAKA RUFAA KUPINGA HUKUMU YA KESI YAKE

Wanasheria wa mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi pamoja na baba yake Jorge Messi wanatarajia kukata rufaa kupinga
hukumu ya kifungo cha miezi 21 jela kinachomkabili nyota huyo wa club ya FC Barcelona pamoja na baba yake kwa madai ya ukwepaji kodi. Kwa mujibu ya mahakama hio ya Uhispania Lionel Mesi alikwepa kodi kiasi cha €4.1 milion kuanzia mwaka 2007-2009. Hata hivyo kwa mujibu wa wanasheria wanadai hukumu hio haimaanishi kua tayari messi anakwenda gerezani moja kwa moja kwani kwa sheria za uhispania kama mtu ameshtakiwa kwenda jela kwa kifungo kisichozidi miaka miwili na hajawahi kushtakiwa kwa makosa mengne hapo kabla adhabu yake inaweza kubadilishwa na mtuhumiwa kulipa faini.

Kwa sababu hio wanasheria hao wamesema wataendelea kuwapigania wateja wao kwani bado wana nafasi ya kuwatetea na hivo kubadili hukumu ya mahakama iliotolewa jana.

No comments:

Post a Comment