Tuesday, 5 July 2016

DONALD TRUMP NA MAREKANI MPYA(Muendelezo)

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya marekani(muendelezo...)


11. Waislamu wote wakataliwe kabisa kuingia Marekani. Yeye anaamini waislamu ndo wanaovuruga amani.

12. Kuwarudisha makwao Wasiria wote wanaoomba hifadhi marekani. Licha mpango huu kukosolewa kila upande lakini ndicho anachokiamini.

13. Dunia ingekua salama zaidi kama Muammar Gaddafi na Saddam Hussein wangekua bado wako hai. Anaona kali nchini Iraq na Libya imekua mbaya zaidi kuliko kipindi ambapo hao viongozi walikua hai.

14. Kama daktari yeyote akipinga utoaji mimba basi aadhibiwe. Kama kutoa mimba kutakua sio halali basi mwanamke alopata mimba aadhibiwe.

15. NATO ni hasara. Kuwepo kwa NATO ni hasara kwa taifa kwani Marekani pekee ndie mchangiaji mkubwa kuliko wengine wote.

16. Mabadiliko ya tabia ya nchi ni "hali ya hewa tu". Anaimini hiki kinachoitwa mabadiliko ya tabia ya nchi sio ni janga lisababishwalo na viwanda bali ni hali ya hewa tu.

17. Kim Davis apangiwe kazi nyingne. Huyu alikua karani wa Kentucky alihukumiwa kwenda jela kutokana na kukataa kutoa cheti cha ndoa kwa mashoga kutokana na imani yake ya kikristo. Trump anasema hata yeye ni muumini mzur wa kikristo ila Kim Davis alipewa kazi isiyo yake.

18. Obama care ni "janga" Trump anaona kua mpango wa afya wa raisi wa sasa n mzigo kwa wengne.

19. Maisha ya wamarekani weusi ni "Shida". Alitoa takwimu akihusisha wazungu waliouawa na wamarekani weusi ni wengi kuliko wamarekani weusi wanaouawa na polisi wa kizungu.

20. Tokyo na Seoul wamapaswa kujenga maghala ya silaha za kinyuklia. Anaona uchokozi wa Korea kaskzini kama tishio kwa nchi hizo za peninsula.

No comments:

Post a Comment