Tuesday, 5 July 2016

MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA KUCHUNGUZWA DAR.

Ndege iliyopotea Malaysia kuchunguzwa nchini


Florence Majani
Bawa mojawapo la ndege hiyo linadaiwa kupatikana hivi karibuni katika Kisiwa cha Kojani,
Pemba na tayari wataalamu wa uchunguzi wa ndege kutoka Malaysia wanatarajia kuja nchini kulichunguza.
Dar es Salaam. Unaikumbuka ndege aina ya Boeing 777 ya Shirika la Ndege la Malaysia, MH 370 iliyopotea Machi 8, 2014?
Bawa mojawapo la ndege hiyo linadaiwa kupatikana hivi karibuni katika Kisiwa cha Kojani, Pemba na tayari wataalamu wa uchunguzi wa ndege kutoka Malaysia wanatarajia kuja nchini kulichunguza.
Mkurugenzi wa Kanuni za Usalama wa Anga wa Mamlaka ya Anga Tanzania (TCAA), Redemptus Bugomola amesema
wachunguzi wa ndege wanakusanya vipande vya bawa hilo tayari kwa uhakiki.

Source: Mwananchi

No comments:

Post a Comment