PILISI WANNE WAUWA NA SABA KUJERUHIWA

Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Maafisa wa polisi katika mji ulio katika jimbo la Texas, wanasema mauaji hayo yametekelezwa na washambuliaji wawili wa kulenga shabaha.
Msako mkali unaendelea kuwasaka washambuliaji hao, mkuu wa polisi wa Dallas David Brown amesema.
Maafisa wengine saba wa polisi wamejeruhiwa, Bw Brown amesema.
Wawili wamefanyiwa upasuaji wa dharura na mmoja yumo katika hali mahututi.
Ufyatuaji risasi ulianza waandamanaji walipokuwa wakipitia barabara za mji na kuwafanya waandamanaji kukimbilia usalama wao.
Maandamano hayo yalitokana na kuuawa kwa wanaume wawili weusi, Philando Castile jimbo la Minnesota na Alton Sterling.

Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU