Monday, 4 July 2016
MWALIMU HUYU ATSTUFAA SISI WANAFUNZI?
Kaspersky:
*SHULE SERIES*
*HEAD MASTER/ MWALIMU MKUU*
*SEHEMU YA KWANZA*
Nakumbuka kwa uzuri kabisa kua siku hio ilikua n nzuri saana, maama niliamka asubuhi na mapema nkavaa sare zang mpyaaa za shule yetu, nilibeba mfuko wangu wa madaftar...na safar ikaiva kwenda kuanza shule rasmi! Nilipofika shule nilipokelewa kwa tabasamu za walimu na wanafunzi pale shuleni. Kila mtu alifurahi kwa kua mda mfupi ndipo shule yetu ilikua imeanzishwa kwa juhudi za mkuu wa shule bwana Rev.Democrat. Kwa kweli mkuu wetu alipendwa saana kutokana na juhud zake za kuipigania shule kwa maslah ya watoto pale kijijin na vijiji vingne vya jirani. Lakin sio km watu wote walikubaliana nae la! Wengne walimpinga. Kutokana na uchanga wa shule tulisoma kiugumu ugumu ila mkuu mara zote alisisitiza kuthubutu, kujiamin na kujitegemea.
Kwa kweli ndoto yake ilikua n kuleta usawa na maendeleo kwa kila mtu lakin haikua kaz rahis, alifanikiwa kwa kias chake lakin sio km alivyoota kua ije kua.
Miaka ilipita shule isonga mbele japo changamoto zilikua nying mwalim mkuu alijarbu kuzitatua kwa kutumia *akili, busara, utashi, weled na maarifa*. Alihimiza kujitoa kwaajili ya wengi.
Nakumbuka siku moja alitukusanya wanafunzi na wazaz/walez akisema kuna jambo alitaka kutuambia.😥😢 Tulifika kwa wingi na kama ilivo ada tulikua na furaha ila baada ya muda mfup hapakua na furaha hata kidogo😢😥, nakumbuka tulikua tumejiinamia hakuna mtu aloweza hata kunong'ona ndipo nilisikia sauti kutoka mbaaal zikijisifia kua *"Tumeshinda! Tumesjinda"* zikiambatana na vicheko vya kejeli. Mwalim mkuu alituambia kua hawez kuendelea kuiongoza shule yetu. Hiki ndicho kilileta huzuni😥. Ningali najiuliza saana juu ya zile sauti na vicheko ni za akina nani? 😳
**~~~**
Siku zilienda mwishowe tukampata *Mwalimu mkuu Mpya* huyu mkuu hakua km yule mwanzo😥🤔 aliamuru shule yetu iandikishe mtoto yeyote bila kujali atokapo.
Nakumbuka siku moja tulikua darasani tukiwa tumejazana saana kwa bahat mbaya mwanafunzi mmoja akajamba! Hali ya hewa ibadilika ikawa mbaya mno tukasukumana na kupiga kelele labda kila mtu avute hewa ya *Oksijeni* japo mara moja😢🤔. Mwalimu mkuu baada ya kuona vile akaamuru tufungue madirisha. Kwa kua darasa letu lilikua ule upande wa choo cha wanafunzi basi *NZI* walimiminika darasan na tuliposema *"Jaman fungeni madirisha!"* mkuu akasema *"Msifunge madirisha kwan nzi wakiingilia upande huu wa kulia watatokea kushoto"*. Niliguna kwa sauti mkuu akageuka na kuniambia *"Nimefanya hivi ili tupate kupumua, tumia mkono na daftar lako kufukuza nzi ila hatutafunga madirisha"*😥😳
Namkumbuka mwali huyu km Mr.FreeAir.
Hakukaa muda sana akaja mwingne...
(Bado nipo shule)
*Itaendelea....*
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment