Kama unamiliki smartphone au kompyuta na unapendelea kuhariri picha zako basi moja kati ya hizi application za kuhariri picha sio za kukosa!! Unaanzaje kukosa kwa mfano??
1. GIMP
Inawezekana jina hili ndo kwanza unaliona leo hapa lakini hii ni photo editor nzuri tuu hasa kwa matumizi kama picha kubwa. Licha ya matatizo madogo madogo bado ni nzuri.(japo kwa wasio wazioefu wanaweza shindwa kuitumia).
2. Paint.NET
Photo editor hii ni nzuri kwani kama unapenda kutumia "layers", "filters" na "plug-ins" ziko za kutosha. Urahisi wa kutumia ndo sifa yake kubwa na pia kama simu yako ina RAM ndogo basi hii itakufaa.
3. PHOTOSPACE
Inauwezo wa kuchukua picha zaidi ya moja na pia unaweza kugawa au kuunganisha picha.
4. GOOGLE NIK COLLECTION
Hii ni "professional level filter selection". Hapa inahitaji ujuzi wa kucheza na filters so kama mgeni utaona kama inaboa ila ukweli ni nzuri.
5. PIXRL
Hii wengi mtakua mnaijua. Ni program ya hali ya juu ya kuhariri picha. Alafu hii hapa unaweza kuhariri picha hata online japo ina changamoto zake katika kuitumia lakini iko vizuri.
6. FOTOR
Hii ni nzuri katika kuunganisha picha. Iko vizuri kuliko.programu zingne japo sio nzuri kwenye kuihariri picha.
7. VINTAGER
Hii pia inafahamika sana miongoni mwa watu kwa kua baadhi ya features zake zinatumika kwenye mitandao ya kijamii kama Instagram.
8. SUMO PAINT.
Ina uwezo mkubwa saana wa kuhariri picha lakini ina vitu vichache saana kuliko matarajio ya wengi.
9. IRFANVIEW
Hii ni programu ya kuangalizia picha (Photo/picture viewer) lakini imeongezewa uwezo wa kubadili na kihariri picha.
10. On 1 EFFECT 10 FREE
Hapa kumbuka ziko mbili kuna hii ya bure na nyingine inaitwa "On 1 Effects 10 proper. Hii ya pili ya kulipia. Iko vizuri sana katika kung'arisha picha na kuifanye iwe na muonekano angavu zaidi.
Kumbuka kuhariri picha sio kufanya "cropping" pekee au kuweka effects tu. Unaweza tengeneza picha nzuri saaana yani. Wewe vipi yako ipo hapo? Comment hapo chini
No comments:
Post a Comment