UINGEREZA KUPUNGUZA KODI KWA MAKAMPUNI.

Uingereza kuvutia makampuni ya biashara

Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake yenye lengo la kupunguza kodi muhimu ya faida katika biashara.
Hatua ya Osborne ni sehemu ya mkakati wa kiuchumi katika harakati za kuvutia uwekezaji mpya, na hii inafuatia kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo iliamua Uingereza isite kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya.
Osborne aliliambia gazeti la Financial Times kwamba anataka kupunguza kodi ya shirikishi kutoka asilimia ishirini hadi chini ya asilimia kumi na tano.mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara ameeleza kwamba kura ya maoni ilikuwa ni mkakati wa kuisaidia Uingereza kuvutia uwekezaji kutoka kwa kampuni mbali mbali mpango ambao inawezekana haukufanikiwa kufuatia kura hiyo ya maoni.

Comments

Popular posts from this blog

HII NDIO HATARI KAMILI KATIKA VITA HUKO UKRAINE. VITA YA TATU YA DUNIA AU VITA VYA NYUKLIA

AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? KWANINI SASA WAAFRIKA WANADAI RAMANI HALISI?

TOP 10 YA SIMU ZENYE KAMERA BORA ZAIDI DUNIANI MPAKA SASA

'MALAIKA' ALIYEIKOA ISRAEL KUANGAMIZWA NA WAARABU