Tuesday, 5 July 2016

TUIGE MFANO WA ETHIOPIA.

Licha ya changamoto za ukame zinazo ikumba Ethiopia lakini bado wana nia ya dhati ya kuifanya Ethiopia kua taifa  na lenye nguvu kiuchumi barani Afrika.

Taifa lolote ambalo lina watu makini, viongozi wenye mawazo ya mbali, waadilifu na waliojitoa huweza kuendelea kwa haraka zaidi kuliko inavodhaniwa.
Kwa miaka mingi sasa Afrika tunakosa nguvu ya kuthubutu kutokana na ubutu wa fikra na mawazo ya ya viongozi wetu. Viongozi wengi wa Afrika wamekua wapga wa kifanya maamuzi magumu na hukimbilia kwenye maamuzi ya kulazimishwa au maamuzi yanayotokana na hisia zao na sio kutokana na ukweli na uhalisia.
Tukiizungumzia Ethiopia kwa upande wake wapo wakusema n nchi inayoongozwa kidikteta na wapo wataosema n demokrasia. Yote yanaweza kua sawa lakini kwa leo mimi napenda niseme kidogo kuhusu maendeleo yao. Nani asiejua mpango wa Ethiopia wa kutaka kuuza umeme aake kwa nchi jirani za Kenya,Sudan na Tanzania?? Nchi gani Afrika mashariki na kati inaweza kujivunia kua na shirika la ndege kubwa na bora kama Ethiopia Airways? Nani leo hii hapa karibu ukitoa Afrika ya kusini anaeweza kujivunia treni za umeme? Hakuna.
Ethiopia ni taifa linalokumbwa na mabalaa ya njaa, na ukame wa mara kwa mara. Lakini licha ya hayo bado Ethiopia uchumi wake unaimarika na kukua kwa kasi. Sasa swali ni je sisi ambao hatuna vikwazo hivyo kwanini hatujilinganishi na Ethiopia? Ukianza kuangalia kwenye mipango yao ya umeme kwa mfano Ethiopia inatarajia kuzalisha zaidi ya megawatt 15,000 ifikapo 2020 kwa kutumia maji, mafuta,upepo, jotoardhi na jua. Ethiopia ni shule mipango yao n darasa na vitendo vyao n somo. Hata sisi tunaweza kwenda shule kujifunza na tukaingia darasani kufundishwa na tukatoka darani tukiwa tumeelewa somo. Simo linaweza kua n moja lakini mitaala itatofautiana kulinganangana na mazingira. Fursa za maendeleo zipo na nia ya kuendelea tunayo kitu kimoja tu tumekosa njia ya maendeleo! Mara nyingi tumekua na project ambazo hazina matunda kama uwekezaji ulofanyika. Leo mtu akikuuliza ni bidhaa au huduma inayoitambulisha Tanzania mtu lazima upate ukakasi kujibu. Hatuna kiupembele kilichojipambanua dhahiri shairi. Kwetu sisi kila kitu ni kipaumbele na inashangaza pale inapokuja hata kipaumbele chenyewe hatuna imani nacho kwani hatuwekezi vya kutosha.

Wito wangu kwa serikali yangu ni kwamba tusihubiri maendeleo bali tuyatende maendeleo. Na dhana yaaendeleo ni pana na inahitaji ushiriki na ushirikishwaji. Maendeleo tunayoyahubiri yawe n maendeleo ya mali, akili na utu. Kama maendeleo yatakuja kwa unyonyaji wa damu za watu basi maendeleo yetu hayana tofauti na maendeleo ya zombie/Vampire. Ili vampire aendelee anapaswa kunyonya damu. Maendeleo ya nchi yaendane na ustawi wa watu katika taifa.

No comments:

Post a Comment