Friday, 8 July 2016
TOP 10 YA VIONGOZI WANAOTUMIA MAGARI YA BEI MBAYA KULIKO
Inaendelea.....
Haya magari ntatoa baadhi ya sifa zake kwa ufupi.
10. INDIA-Mercedes Benz Pullman Guard
•Anaitumia Narendra
Mondi
Ina kinga dhidi ya maguruneti na risasi.
Ina eneo lake maalum ambalo ni tofaut na maeneo mengne ndani ya gari.
Ina viti na muonekano classic.
Inatumia mfumo wa GPS na satellite.
Thamani yake ni $180,000(414Mil)
9. PHILIPPINES-Mercedes Benz W221
Mmh
Ina engine ya nyota 5 katika performance.
4 door
Sensor kwaajili ya kuhisi ajali inayokaribia!(hasa inayoweza kusababishwa na kugongana).
Ina mfumo wa kujilinda wa kielekroniki
Ina vitu vingi vya kifahari ndani
Ina mfumo wa radar na mambo kibao ya kufurahisha.
Ina brake assist.... Yaan gar iko full equipped.
Thamani yake $ 250, 547(576.25Mil).
8. RUSSIA Mercedes Benz S-Class Limousine
Gari ya mtu mzima raisi Putin. Hafanyi mchezo aisee! Alichagua design ya kipee ya limousine.
Ina ulinzi mkali dhidi ya mabomu na risasi.
Ni gari flani fupi kwa kima lakini ni ndefu kiasi kwa ulalo.
Ndani ni mwendo wa leather tuu!!
Thamani yake ni $251,417(578.3Mil)
7. MALAYSIA-Maybach 62
Ina viti vya kuzunguka ndani, vitu vya usalama, meza za "bata". Ina vitu vuzuri vingi saana.
Thamani yake ni $394,000(906.2Mil)
6. UINGEREZA-Jargur XJ Sentiel
Anatumia wazuri mkuu wa uingereza.
Bonge moja ya gari kutoka Jaguar ina vifaa vya usalama full, supercharged 5-liter V8 engine. Bodi yake imetengenezwa kwa titanium, chuma..ili kuzuia risasi. Ina mfumo wa oksejeni kama ikitokea janga. Pia ina mfumo wa kuzuia gesi ya machozi kupenya.
Ina mifumo bora ya sauti kwaajili ya kufanya mikutano akiwa njiani, ina tv za high definition.. N.k
Thamani yake ni $455,025(1.04bilion)
5.THAILAND-Maynach 62 Limousine.
Anaitumia king Bhumibol Adulyadej
Gari ina muundo flani wa kistarehe zaidi, ina mfumo wa DVD na CD na inatumia mifumo yote ya kisasa ya ulinzi na usalama.
Thamani yake ni $500,000(1.15bilion)
4. VATICAN-Mercedes Benz M-Class
Anaitumia papa Francis(popemobile)
Ina muundo wa kipekee lakini pia ulinzi ni wa maana. Speed yake inaweza kufika 160miles/hr
Thaman yake ni $524,990(1.2bilion)
3. CHINA-The Hongqi Limousine
Kwanza hilo jina lina maana ya "bendera nyekundu".
Ndio gari ghali zaidi nchini china. Asee hii gari ni hatari ina 8 speed transmission, 4 turbo charged V8 engines na horsepower 381.
Speed ya juu ni 220km/hr.
Thamani yake ni $801,624 (1.84bilion)
2. USA-Cardillac One
Asa sikia!!
Hii gari huitwa "The beast"
Anatembelea Obama.
Inatengenezwa na General motors lakini na wana intelijensia wa marekani.
Ina sehemu ya kufanyika mkutano na pia hairusu mawasiliano ya simu kuingia kwa mtu mwngne ila kwa raisi tu. Na mawasiliano lazma yatoke state house. Alaf ina sensor ya kugundua aina ya damu raisi na pia ina mfumo wa oksijeni kama likitokea tatzo. Gari hii kama ikichoka basi wanaintelijensia wa marekani wanapaswa kuilipua.
Thaman yake ni $1, 500,000(3.56bilion)
No oneeee 1!!
QUEEN OF ENGLAND-Bentley State Limousine.
Asa hii gari n kufuru asee. Kumbuka ni familia ya kifalme..
Ilitengenezwa kipindi kampuni hio ilikua inatimiza miaka 50.
Ina kila kitu ambacho kama mke wa mfalme anataka.(yaani mle ndani vitu bya dhahabu na madini mengne ya thamani).
Kwa kua kipindi inatengenezwa malkia alikua na miaka 90 basi na vioo vya madirisha vinafunguka kwa 90°!! This is amazing. Hakuna kiongozi uingereza atatembeza kigari chake ikionekana gari hii mtaani!!
Thamani yake ni $ 15,167,500(34.8bilion)
(Ina thamani mara 10 zaidi ya "The beast" gari ya raisi wa marekani Barack Obama).
Na pia ukijumlisha thamani ya magari ya viongozi hawa 10 Wa juu huwezi kuinunua gari ya Queen Elizabet.
(Hizi pesa zimebadilishwa kwa viwango vya sasa vya dollar).
Na hio inaweza kununu hata ndege!!
Ukitaka kusema chochote comment yako ihusike hapo chini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment