AFRIKA NI KUBWA KIASI GANI? HATIMAYE AFRIKA IMEANZA KUZINDUKA. Ramani ya dunia Tulipokua shuleni tulijifunza mengi juu ya Afrika lakini mengi ilikua ni upotoshaji wa kukusudia au kutokukusudia. Hilo linajidhihirisha pale unapotazama ramani ya dunia. Utaambiwa Afrika ni bara la pili kwa ukubwa duniani nyuma ya Asia lakini ukitazama ramani utagundua Amerika ya Kaskazini inaonekana kuwa ni kubwa kuliko Afrika. Lakini je Afrika ina ukubwa gani? Na kwanini sasa Umoja wa Afrika unahitaji taasisi kuu ulimwenguni kote kutumia ramani mpya ya Afrika kulikoni? Tunarejea takribani miaka 456 hivi nyuma kuanzia sasa. Tunakutana na mwaka 1569, na hapo tunakuja kukutana na mtu mmoja aliyepata kua ni mwanajiografia na mchora ramani kutoka Flanders (Kijiografia eneo hili liko Ubelgiji na kijamii na kiutamaduni limekaliwa na watu asili ya Wadachi). Mtu huyu alitwa Gerardus Mercator ambaye ndiye aliyechora ramani hii ya dunia ambayo katika karne ya 18 ilirasmishwa kutumika katika maswala ya usa...
Comments
Post a Comment