Sunday, 23 October 2016

KUTANA NA MARAIS "VIPANGA"KUTOKA AFRIKA.

KUTANA NA MARAIS WALIO BUKUA KWA SANA(VIPANGA) KUTOKA AFRIKA.

Sio tu kua hawa viongozi wana nguvu na ushawishi kisiasa bali ukiangalia taaluma zao pia ziko juu sana. Wana weledi mkubwa kitaaluma na hawa wanatuthibitishia ule msemo wa kiingereza usemao "readers are leaders". Orodha hii imepangwa kulingana na vigezo vyao vya kitaaluma.

Saturday, 22 October 2016

NCHI ZINAZOONGOZA KUA NA "VIPANGA" SHULENI.

Katika kutathmini viwango vya elimu duniani, wengi wamekuwa wakiangazia sana ubora wa vyuo. Lakini kwa jumla, ni mataifa gani yenye wanafunzi walio bora zaidi?

Friday, 14 October 2016

NCHI ZINAZOONGOZA KWA AMANI AFRIKA.


Kulingana na Global peace index 2016 wametoa orodha ya mataifa yanayoongoza kwa amani duniani. Nchi hizi zimepangwa kulingana na viashiria vikubwa vitatu: kiwango cha ulinzi, usalama na kiwango cha migogoro ya ndani na nje ya nchi na pia nguvu za kijeshi.

Thursday, 13 October 2016

MWANAFUNZI ATENGENEZA BOMU LA MACHOZI,

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda amevumbua njia ya kutengeneza mabomu ya kutoa machozi ambayo hutumika na vikosi vya Polisi mara nyingi kuzima maandamano.

Tuesday, 11 October 2016

JENGO LA JULIUS NYERERE LAFUNGULIWA RASMI ETHIOPIA.


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Julius Nyerere.

Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.
Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).

Monday, 10 October 2016

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.

KIZUNGUMKUTI CHA SAKATA LA MBEYA DAY.

Kwanza nipende kuwapongeza watanzania wote kwa ujumla kwa jinsi ambavyo naona swala la teknolojia ya habari na mawasiliano limeweza kua ni chachu ya mabadiliko hapa nchini. Na kama tutaendelea kua na weledi wa matumuzi bora ya maendeleo haya ya sayansi na teknolojia basi, naamini tutafika mbali. **

Friday, 23 September 2016

Sunday, 18 September 2016

PICHA 10 AMBAZO HUWEZI KUAMINI KAMA NI ZA KUCHORWA

Huko Accra, Ghana anaishi kijana mmoja ambae maajabu yake makubwa yapo katika matumizi ya kalamu ya risasi "Pencil". Jina lake maarufu anaitwa Theopencil kutokana na matumizi yake ya kalamu.

Saturday, 20 August 2016

SHETANI ALIANZA LINI KUA SHETANI?

SHETANI ALIANZA LINI KUA SHETANI?

Hakika sifuri(0) sio sawa na o. Sifuri ni tarakimu lakini o ni herufi. Sifuri na o zinataka kufanana lakini hakuna hata siku moja sifuri iwe o na o iwe sifuri. Huo uwezekano haupo. O itabaki kua O na 0 itabaki kua 0. Wakati fulani tumekua na mazoea ya kutaka kulazimisha vitu vinavyofanana viwe sawasawa. Kufanana hakuna maana ni sawa sawa.

Friday, 19 August 2016

POGBA KUKIPIGA DHIDI YA SOUTHAMPTON

Mourinho: Pogba atacheza dhidi ya Southampton.

TRUMP APATA PIGO BAADA YA KUJIUZULU KWA MWENYEKITI WA KAMPENI.

Mwenyekiti wa kampeni ya Trump ajiuzulu


Mwenyekiti ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amejiuzulu miezi miwili tu baada ya kushika usukani.
Alichukua nafasi hiyo kama mwenyekiti wa kampeni, baada ya meneja wa zamani Corey Lewandowski kufutwa kazi mwezi Juni.

Tuesday, 16 August 2016

JUSTIN BIEBER AFUTA ACCOUNT YAKE INSTAGRAM, KISA DUUH!!!

Justin Bieber kafuta account yake ya Instagram yenye followers mil 77.8, kisa

Justin Bieber ambaye ni star aliyeanza muziki akiwa na umri mdogo na mpaka sasa anafanya vizuri katika game ameingia kwenye headlines baada ya kufuta account yake ya Instagram ambayo ilikuwa na followers milioni
77.8 .

MAMA WA USAIN BOLT AMTAKA MWANAE ATAFUTE MKE.










Usain Bolt akiwa na mama yake wakishangilia moja ya ushindi wake.

MAMA YAKE USAIN BOLT AMTAKA MWANAE KUOA.

Saturday, 13 August 2016

RAISI MAGUFULI AMKUBALI MRISHO MPOTO


Utunzi mahiri wa mashairi na ughani uliotukuka wa Mrisho Mpoto, umeligusa sikio la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ameeleza kuwa shabiki mkubwa wa kazi za msanii huyo hususan wimbo wake ‘Sizonje’.

MESI AKUBALI KURUDI TIMU YA TAIFA.


Nyota na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Mesi ameamua kubadili uamuzi wake wa kustaafu kuichezea timu yake ya Argentina kufuatia matokeo mabovu ya timu yake kwenye fainali za michuano mikubwa. Mesi alifikia uamuzi huo kufuatia mazungumzo kati yake na kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza.

Thursday, 11 August 2016

HAKUNA "UBINAMU" NCHINI KENYA WANAKULAGA!

Mahakama ya juu nchini Kenya imehalalisha uhusiano wa kimapenzi baina ya mabinamu kwa sababu inakubalika katika baadhi ya jamii nchini humo.

Wednesday, 10 August 2016

SIFA 5 ZINAZOKUONESHA KUA WEWE NI "SMART" KULIKO WENZAKO.

KAMA UNA VITU HIVI JUA WEWE UKO SMART KULIKO WENGINE.

Wanasayansi wamegundua vitu vitano vinavyoonesha kua wewe ni smart kuliko wengine.

1. Mtu anaetumia mkono wa kushoto(Left handed).
Ni zawadi ya ubunifu ulopewa tangu kipindi unazaliwa. Watu wanaotumia mkono wa kushoto wana maamuzi ya haraka kuliko wale wa kawaida(mkono wa kulia).

2. Mcheshi(sense of humor)
Kuna utafiti ulifanywa karne ya kumi na saba na ulionesha kua wachekeshaji wa IQ kubwa kuliko wengine.

3. Mzaliwa wa kwanza
Zamani ilikua mzaliwa wa kwanza anapewa urithi mara mbili ya wengine kwa kutambua thamani yake. Hata sasa wazaliwa wa kwanza wanaheshimika kwani wao ndio kioo cha ndugu zake wanaomfuata.

4. Kuchelewa kuamka
Wanasayansi wamegundua kua kua wale wote wanaochelewa kuamka ni bora kuliko wale wanaodamka asubuhi na mapema.

5. Introvert (Mndani)
Huyu ni mtu anaetegemea sana uwezo au vyanzo vya ndani kwaajili ya maendeleo yake. Zaidi 60% ya watoto wenye vipaji ni introvert. Wanatumia walivyo navyo ndani kuliko vilivyo nje.

Kwa sifa hizi je wewe ni smart kuliko wengine????

MASOMO YA SAYANSI NI LAZIMA KWA WANAFUNZI WOTE.







Waziri wa Elimu, Teknolojia, Sayansi na Mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako.

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya kuwa kuanzia sasa masomo ya sayansi ni lazima kusomwa na wanafunzi wote wanaosoma elimu ya sekondari kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Kwa mujibu wa Sera ya Elimu iliyopo, wanafunzi wanaosoma elimu ya sekondari wanaweza kuchagua aina ya masomo watakayo wafikapo kidato cha tatu na kuacha mengine.

HATARI TANO USIZOZIJUA KUHUSU SIMU YAKO.

MADHARA YA SIMU AMBAYO HUJAWAHI KUAMBIWA.


Kwa miaka mingi sasa kumekua na mijadala mikubwa kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya simu. Matumizi ya simu yamekua yakiongezeka kila kukicha. Sasa watu wanatuma ujumbe wa maneno, sauti,video, kuchati kwenye mitandao ya kijamii, kutazama video mtandaoni, kutumiana picha, kuperuzi, kusoma vitabu, majarida n.k kupiga picha za selfie n.k yote haya ni matumizi ya simu lakini swali kubwa linabaki "Je ni kweli matumizi ya simu hayana athari zozote kiafya?".

Sunday, 7 August 2016

TAARIFA RASMI YA MAN UNITED JUU YÀ POGBA












Ni taarifa iliyotolewa na manchester united kupitia tofuti yao. 

Headlines za kiungo wa kimataifa wa Ufaransa aliyekuwa anaichezea klabu ya Juventus ya Italia Paul Pogba kuhusishwa kujiunga na Man United, zinaelekea kumalizika kwa kiungo huyo kurudi Man United toka aondoke mwaka 2012.

Wednesday, 3 August 2016

RAISI AMTEUA MKEWE KUA MGOMBEA MWENZA



Managua. Rais wa Nicaragua, Daniel Ortega amemtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwingine.

Tuesday, 2 August 2016

WATAWALA WA SHERIA AU UTAWALA WA SHERIA??

UTAWALA WA SHERIA vs WATAWALA WA SHERIA.

Hiki kichwa cha habari niliona kikiwa kwenye lugha ya kingereza. Ni kitabu kilichoandikwa na Prof. Issah Shivji akielezea maisha ya Jaji mkuu mstaafu Barnabas Albert Sammata. Nilipenda kukisoma kitabu hiki lakini sikufanikiwa. Ila nilifanikiwa kupata dhima ya juu ya kitabu. Lakini nilipenda maneno machache tu ya jaji samata ambayo nami ntayatumia hapa.
Aliwahi kusema "Let everyone in our society give justice a chance to prevail".(Hebu tufanye kila mmoja wetu katika jamii aipe haki nafasi ya kukua"[tafsri sio rasmi]).

Katika taifa lolote lile litakalokua linajiita ni taifa la kidemokrasia basi halina budi kuruhusu ustawi wa haki. Na haki itakuepo pale tu ambapo watu waliopewa dhamana ya kuisimamia wanakua na maadili. Amini usiamini ila kuna kazi hazihitaji saana maadili kama zingine.

Uongozi ni kazi ambayo huwezi kuifanya kama huna maadili. Wanasaikolojia wanaamini ili kuweza kumjua mtu alivyo ni lazma tumjue kupitia tabia. Tabia ni matendo ya nje ya mtu yanayodhihirisha namna alivyo kwa ndani(fikra, maono,imani yake ya ndani). Sasa mtu anachokiongea na kukifanya kwa dhamira jua ndivyo alivyo(awazavyo mtu ndivyo alivyo).

Sasa basi tumeshaona matendo ya viongozi wetu, wameonesha dhamira zao za ndani, imani na mitazamo yao imeoneshwa kwa kauli na matendo yao. Mwanzo nilidhani ni mapitio lakini sasa naamini ni dhamira zao. Hadi sasa kuna nafasi finyu ya kusema demokrasia haijateteleka; utawala wa sheria unaheshimiwa. Ni rahisi kusema kuna utawala wa sheria lakini utapata shida kudhihirisha kwani mifano halisi iliyopo  inapingana na demokrasia; inapingana na utawala wa sheria. Karne hii ni karne ya kuzuia Bunge(chombo cha wananchi) kurusha matangazo ya papo kwa hapo? Kuwakataza na au kuwahukumu mawakili wanaohitolea kuwatetea wananchi? (c'mon tuko serious kiasi gani??), kuzuia mikutano ya kisiasa kwa sababu ambazo kwa akili ya kawaida zina walakini. Taifa limetumbukia kwenye tatizo kubwa la kauli reja reja! Kauli hazina msingi wala nguzo ya kikatiba au kisheria. Haijalishi tunatamani maendeleo kwa kiasi gani lakini isiwe ndio tiketi ya kuangamiza utu na uhuru wa mwananchi, isiwe ndiyo tiketi ya dhulma na utawala usiofuata sheria. Kwa yanayoendelea nalazimika kuamini kua kwa sasa tayari kuna watu wanaogopwa na sheri(kuna mazingira sheria inaogopa watu). Naamini bado kuna upofu wa kisiasa. Tujue na tulmelewe kabisa kua siasa na maisha havitenganishwi hata kidogo. Kauli ya kiongozi wa kisiasa ina athari kubwa kwa jamii kwani wao wana ushawushi kwa watu wao hivyo kauli yeyote iliyokinyume na matakwa ya jamii husika ni wazi kua italeta madhara hasi nengi na mwisho wa siku labda litapelekea 'anguko la kijamii'. Kupitia kauli utapanda  chuki au upendo, utapanda wema au uovu, utapanda woga au kujiamini. Na falsafa ya maisha na uongozi wa sasa ndio falsafa ya viongozumi wa baadae kwani ndicho kinachojengeka akilini mwa watu wa sasa.
Ila naanini historia inakwenda kwa mfumo wa mawimbi(waves). Na siku zote tunasoma historia lakini hatuelewi. Tulipaswa kujifunza kupitia historia ili kutoruhusu makosa yale yale kurudiwa katika hali na mazingira yale yale.Na hii tabia ya historia inafanya historia kujirudia. Nakumbuka historia ya Adolf Hittler alipoitwaa ujerumani rasmi mwanzoni mwa 1930s, nakumbuka mengi na makubwa aliyafanya ila mwisho wa siku alijichimbia kaburi na kuiacha Ujerumani ikiwa kama mkiwa huku ikinyoshewa vidole vya ubaya.

Hakuna namna yoyote sisi tunaweza kujisifu kua tumepiga hatua katika demokrasia. Bado tungali tumenasa katika tope la fikra zilizofubaa; mawazo mgando na mitazamo hasi. Tunakimbia mbio kuelekea uelekeo tusioujua tukiamini kua kutafika salama! Hivi ni nani aliyeturoga?? Mchawi wa kwanza ni mimi(ninayesoma hapa). Na hatuna cha kujivuna kama maendeleo yetu yatakua juu ya kafara za watu wetu. Ulishawahi jiuliza nani aliifanya North America na Ulaya kua kama ilivyo leo?? Nabi alikua kafara??

Demokrasia ya danganya toto na ya woga ndiyo iliyotawala barani Afrika hadi nashangaa kuona pia baadhi ya ya watu wakiiona nchi yetu kama nchi iliyopiga hatua kidokrasia. Na yeyote aitazamaye Tanzania kama nchi iliyokomaa kidemokrsia basi yeye na taifa lake watakua wametumbukia katika lindi la mauti ya fikra, wanaishi kwa fikra mfu na huo ni mwanzo wa anguko la nchi hiyo katika dhambi ya dhuluma ya haki kwa maana huwezi kubali kipofu kuongoza njia tena akiwa hana kifaa chochote. Huo ni uchawi. Sasa hatuwezi ongoza taasisi au nchi kwa kutumia mazingaombwe. Lazima tujikane tuoneshe dhamira zetu za ukombozi kwa kuheshimu haki na utu wa mtu. "Maendeleo ya vitu bila mtu ni upuuzi na batili". Na hakuna maendeleo bila HAKI NA UHURU. Haki na Uhuru ndo viungo thabiti vya dhana nzima ya maendeleo. Acha watu wawe huru na ukiwa huru utaishi kwa amani. Ni muda wa kuanza kufikiri upya, ni muda wa kujitathimini, kujikosoa na kujisahihisha. Tunahitaji maendeleo ya vitu na watu. Kuna faida gani kua na shule, hospitali zilizo kama magereza? Kuna faida gani kua na barabara nzuri kama tutakua hatupiti? Fikiria nje ya sanduku nyeusi(Black box).


Sunday, 31 July 2016

JARIBIO LA KUKUONESHA KAMA HUYO ULIYE NAYE ATAKUA MME MZURI KWAKO.

Jaribio muhimu kujua kama kweli atakua mume mwema kwako.
Ndoa ni safari ndefu na ni muhimu kwa watu kuchagua wenza wao wa maisha ili waweze kuishi nao. Kuna maswali muhimu unapaswa kujiuliza kuhusu huyo mme wako wa baadae ili kujua mahusiano yenu yanaweza kwenda mbali kiasi gani. Kuna viashiria vinaweza kukuonesha ni kipi unaweza kukipata baada ya wewe kumkubali huyo uanaemfikiria kua awe mmeo.

Tuesday, 26 July 2016

MATAIFA YENYE WATU WAREFU ZAIDI DUNIANI.

Utafiti mpya umeonesha kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake, wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.
Kimo cha wastani kwa wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimeta 183), na kimo cha wastani kwa wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimeta 170).

KOFFI OLOMIDE ATAMATWA DR CONGO


Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
Mwandishi wa BBC Poly Muzalia anasema mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la afisi ya mwendesha mashtaka.

JINA LA CHRISTIANO RONALDO KUTAWALA VITU VYA MJI WAKE WA NYUMBANI.


Uwanja wa ndege wa mji wa nyumbani kwa mwanasoka bora mara tatu wa dunia kupewa jina lake ili kuuenzi mchango wake katika soka la nchi hio.

MPASUKO NA SINTOFAHAMU NDANI YA CHAMA CHA DEMOCRAT


Kiongozi wa Chama cha Democratic nchini Marekani amesema atajiuzulu baada ya barua pepe zilizofichuliwa na kuchapishwa na mtandao wa WikiLeaks kudokeza huenda maafisa wakuu wa chama walijaribu kuvuruga kampeni ya Bernie Sanders.

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATOA LA MOYONI.

TAMKO MTANDAO WA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU KUKEMEA UKIUKWAJI WA HAKI ZA WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU NA KUZUILIWA KWA MAWAKILI KUFANYA KAZI ZAO
UTANGULIZI

HUKUMU ILIYOTOLEWA NA MAHAKAMA KUU JUU YA KESI YA DAUDI MWANGOSI.

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Iringa imemtia hatiani askari Polisi Pacificius Cleophace Simoni kwa kosa la mauaji ya bila kukusudia ya mwanahabari Daudi Mwangosi yaliyotokea Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Sunday, 24 July 2016

MOYES APATA KIBARUA SUNDERLAND

OFFICIAL: SUNDERLAND WAMTHIBITISHA MOYES KUA KOCHA MPYA.



Kocha wa zamani wa vilabu vya Everton, Manchester united na Real Sociedad ametangazwa rasmi kua kocha mkuu wa paka weusi (klabu ya soka ya Sunderland) kuchukua mikoba iliyoachwa na Sam Allardeyce ambaye analwenda kuifundisha timu ya taifa ya England (Simba watatu).

NDEGE INAYOWEZA KUPAA NA KUTUA MAJINI.


China imeunda ndege kubwa zaidi duniani ambayo ina uwezo wa kupaa au kutua kwenye maji au uwanja wa ndege.
Ikizinduliwa ndege hiyo ilishangiliwa na umati wa watu katika mkoa ulio kusini wa Guangdong.

MBARONI KWA KUTAKA KUIBA MWNGE WA OLYMPIC.

Polisi nchini Brazil, wamemtia mbaroni mtu mmoja ambaye alijaribu kuiba mwenge wa Olimpiki, ilipokuwa ikipitishwa katika jimbo la Sao Paulo.

KOFFI OLOMIDE ATIMULIWA KENYA NA VISA YAKE KUFUTILIWA MBALI


Mwanamuziki maarufu wa asili ya Congo, Koffi Olomide, siku ya Jumamosi alifukuzwa kutoka Kenya na serikali ya nchi hiyo baada video iliyomuonyesha akimpiga teke mmoja wa wacheza densi wake kulaaniwa vikali, hususan na Wakenya mitandaoni.

WAVULANA WATINGA SKETI SHULENI.

Wavulana wanne katika shule moja nchini Uingereza wamefika shuleni wakiwa wamevalia sketi kulalamikia hatua ya mwalimu kuwaadhibu kwa kuvalia kaptura siku yenye joto kali zaidi nchini humo.

Saturday, 23 July 2016

KIJANA MMOJA AUWA KWA KUPIGWA NA MWEKEZAJI.



















Kijana mmoja aliyejukikana kwa jina moja (Elisha) mkazi wa Kabindi Mkoani Geita amefariki Dunia baada ya kupigwa na mchina kwa jina "Mr. Swii" kwa madai ya kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara. Taarifa zinadai waliopigwa wengine wawili wako hospitali kwa matibabu zaidi.

WALINZI ZAIDI YA 300 WA KIKOSI CHA KUMLINDA RAISI KUKAMATWA UTURUKI.

Uturuki imetoa warrant wa kukamatwa kwa zaidi ya walinzi 300 wa kikosi cha kumlinda raisi kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli tarehe 15 July 2016.
Inasemekana tayari walinzi 283 tayari wameshakamatwa na operesheni hio ingali bado inaendelea, liliripoti shirika la habari la Xinhua.

MLEMAVU APANDIKIZWA MIKONO YA MTU MWINGINE.

Uingereza imefanikiwa kufanya upasuaji na kumpandikiza mgonjwa mikono ya mtu mwingine.
Oparesheni hiyo imefanyika katika hospitali kuu ya Leeds ambako mgonjwa mwenyewe amesema amefurahia kurudishiwa viungo hivyo muhimu mwilini.

Friday, 22 July 2016

ULIIKOSA HII YA KOFFI OLAMIDE AKIMPIGA TEKE DENSA WAKE?

Msanii Koffi Olamide amenaswa na kamera akimpiga teke densa wake wakati wanawasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini kenya.

MAGARI YA UMEME YAANZA KUUZWA KENYA.


Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.

VYUO VILIVYOFUNGIWA KUDAHILI WANAFUNZI KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017


Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetoa orodha ya vyuo ambavyo havitaruhusiwa kudahili wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2016/17.

JE, TUNAWEZA KUEPUKA MALARIA KWA KUFUGA KUKU? SOMA UTAFITI HU.

Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria ?
Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha,, Fuga kuku !
Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.

MAALIM SEIF KUTINGA MAHAKAMA YA ICC


Wakati polisi wakisema wanasubiri jalada la Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad litoke kwa Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) ili wamfikishe mahakamani kwa uchochezi, leo atakwenda katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa (ICC) kuwashtaki viongozi wa Serikali.

Wednesday, 20 July 2016

HATMA YA WANAFUNZI WALIOFULUZWA DODOMA

Kati ya wanafunzi elfu saba (7802) waliokuwa wamejiunga na chuo kikuu cha Dodoma Tanzania ni wanafunzi 382 pekee wenye sifa zitakazowaruhusu kurejea chuoni humo.

WANAWAKE WAOMBA WATAFUTIWE WANAUME WA KUWAOA.

Zaidi ya wanawake waislamu 10,000 wameomba watafutiwe waume watakaowaoa.

Tuesday, 19 July 2016

MKE WA TRUMP KWENYE KASHFA YA WIZI WA MANENO/WAZO.

Wizi wa maandishi wautia kiwingu mkutano wa Republikan
Donald Trump anakabiliwa na kashfa ya wizi wa maandishi au mawazo iliochafuwa hotuba ya mke wake Melanie katika mkutano mkuu wa chama cha Repuplican ambao ufunguzi wake umekumbwa na vurugu za wanachama wa kawaida.

MVUTANO WAZUKA KWENYE SIKU YA KWANZA YA MKUTANO WA CHAMA CHA REPUBLICAN.

Ghasia zatokea kwenye siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa chama cha Republican hapo jana baada ya wakuu wa chama kuzuia juhudi za dakika za mwisho za kubadili kanuni za mkutano.
Hoja ya kutaka wajumbe wapewa nafasi ya kuamua nani wanampendelea kumpigia kura badala ya kumchagua mshindi wa uchaguzi wa awali iliwasiloishwa na kundi linalompinda Trump.

NANI KUA MWANASOKA BORA KWA MWAKA HUU?

Shirikisho la soka barani Ulaya limetangaza majina ya wachezaji 10 watakaowania tuzo ya mchezaji bora Ulaya kwa msimu wa mwaka 2015/2016, majina hayo 10 yametangazwa huku Cristiano Ronaldo akipewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo itakayotolewa Agosti 25 mwaka huu.

TOP 10 YA SIMU KALI ZILIZO SOKONI MPAKA SASA

Kila mtu anapenda kutumia kilicho bora zaidi. Sasa hapa nina orodha ya simu kali zilizoko sokoni mpka sasa 2016. Kama humiliki moja kati ya hizi....daah.

Monday, 18 July 2016

MWALIMU MKUU SEHEMU YA TATU(..3)

MWALIMU MKUU/ HEADMASTER 

SEHEMU YA TATU

Baadae nilimskia mwalimu mkuu kua anataka kupumzika...kila mwamafunzi alifurahi kwa kua aliamini atasoma kwenye shule aliyokua akiiota..

Endelea...

OMBI LA OBAMA KWA WAMAREKANI


Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.

MKUTANO MKUU WA CHAMA CHA REPUBLICAN KUANZA LEO.














Jukwaa litakalokutumiwa na mgombea wa uraisi.

Maelfu ya wanachama na wajumbe wa chama cha Republican nchini Marekani wanakusanyika katika mji wa Cleveland, Ohio, katika mkutano mkuu wa uteuzi wa chama hicho ambapo watakmteua rasmi bilionea Donald Trump kuwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Sunday, 17 July 2016

SABABU ZA UFARANSA KUANDAMWA NA MAGAIDI.

Sera za ndani na nje  za ufaransa zaigeuza muhanga wa mashambulizi. 
Baada ya mashambulizi mawili yaliyouwa watu 17 mjini Paris mwezi Januari 2015, gazeti la Dar al-Salaam linalomilikuwa na "Dola la Kiislamu" (IS) lilichapisha Mnara wa Eifell likiandika "Allah ilaani Ufaransa."

WAAFRIKA SASA KUA NA HATI MOJA YA KUSAFIRIA.


Je unamiliki cheti cha kusafiria cha taifa lako?
Hivi Karibuni, itakuwa hauhitaji cheti hicho madamu wewe ni mwafrika !
Kisa na maana ,,,, Bara la Afrika limezindua rasmi cheti chake cha kusafiria!
Marekani imeitaka Uturuki kujizuia baada ya jaribio la mapinduzi lililozimwa siku ya Ijumaa ambapo maelfu ya maafisa wa kijeshi wamekamatwa.

UFAFANUZI WA TCU JUU YA VIWANGO VYA UDAHILI.

Kufuatia tangazo lililotolewa na tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) wiki iliyopita kumekua na sintofahamu miongoni mwa wadau na wanafunzi juu ya sifa na vigezo vitakavyotumika kwenye udahili kwa mwaka wa masomo 2016/2017. Mapema wiki iliyopita TCU ilibanisha kua ili kujiunga na chuo lazima uwe na alama D ambazo ni pointi 4.

Saturday, 16 July 2016

RIO FERDINAND AITOLEA MATE KAZI YA UKOCHA KUINOA ENGLAND.

Rio Ferdinand anaitamani kazi ya kukukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England maarufu kama "Simba watatu".

MISTARI YA KENDRICK LAMAR KWENYE MTIHANI WA CHUO.

Sasa hivi mistari ya wanamuziki imeanza kutumika kwenye mtihani. Wanafunzi wa chuo kikuu cha Strathmore walishikwa na butwaa baada ya kuingia kwenye chumba cha mtihani na kukutana swali ambalo lilikua na mistari kutoka kwenye wimbo wa Kendrick Lamar

SERIKALI YAKANUSHA KUA INATAKA KUFUTA POSHO ZA MADAKTARI.

Serikali yakanusha kukata posho za madaktari.
Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na Uvumi katika Mitandao ya Kijamii kuwa Serikali imeamua kushusha Mishahara ya Madaktari kwa asilimia 30% ili kuendana na dhana ya Hapa kazi tu na kuwa Serikali imekusudia kufuta malipo ya Posho za Wataalamu wa Afya walio katika Mafunzo kwa Vitendo ufafanuzi kwa Umma wa Watanzania na Watumishi wa Sekta ya Afya kuwa taarifa hizo siyo za kweli.

MAPINDUZI YA KIJESHI NCHI UTURUKI

Kundi moja la kijeshi nchini Uturuki linasema limechukua udhibiti wa nchi, huku madaraja jijini Istanbul yakifungwa na ndege za kijeshi zikionekana kupaa katika anga ya Ankara.

Friday, 15 July 2016

MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016 YATANGAZWA

Kuangalia matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2016 ingia kwenye hii link hapa………>>>http://www.necta.go.tz/results2016/ACSEE2016/index.htm

CHADEMA KUTOKUZUIA MKUTANO WA CCM

Sumbawanga. Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Mkoa wa Rukwa limetangaza kuwa hawatakwenda kuzuia Mkutano Mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Julai 23 mjini Dodoma.

JUVENTUS WAMNASA GONZALO HIGUAIN

Juventus wafikia makubaliano na mpachika mabao wa Napoli, Higuain.
Mabingwa wa Italia wamefanya makubaliano ya mkataba wa miaka minne na kiungo wa Napoli Gonzalo Higuain wenye thamani ya Euro milioni saba(€7milion) kwa msimu kwa mujibu wa mtandao wa goal.com.

SHAMBULIO LAUA ZAIDI YA WATU 80 NCHINI UFARANSA.

Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa.

Thursday, 14 July 2016

ORODHA YA CLUB TAJIRI ZAIDI DUNIANIA


Hii ni orodha ya vilabu 10 vyenye thamani kubwa zaidi duniani kwa sasa. Orodha hii imetolewa na jarida la Forbes.

MAONI KUHUSU WALIMU KUKATWA MSHAHARA JUU YA MADAWATI

WALIMU KUKATWA MISHAHARA KWA SHULE AMBAZO WANAFUNZI WATAVUNJA MADAWATI.

Nikifuatilia kauli za serikali kwa mwaka 2016 sishangai saana kuona kauli hii ikitoka. Inaumiza saana kwa wenye taaluma ya ualimu lakini licha ya mchango mkubwa wa mwalimu kumbukeni huko nje jamii ndo inavowachukulia. Yaani mwalimu unaweza kusemwa kwa vyovyote vile na watu wengi wakaona sawa.

THERESA MAY WAZIRI MKUU MPYA WA UINGEREZA.

Bi Theresa May amechukua usukani kama waziri mkuu wa Uingereza.
Akizungumza baada ya kupokea ufungua wa makao rasmi ya waziri mkuu wa Uingereza 10 Downing Street bi May

Wednesday, 13 July 2016

Hii ni orodha ya nchi zenye kiwango kiwango kidogo cha rushwa na zile zenye kiwango cha juu kabisa cha rushwa duniani. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa shirika la Transparency International (TI) na taarifa na orodha kamili inapatikana kwenye tovuti yao.

UJERUMANI YATAMBUA RASMI MAUAJI YA WAHERERO KAMA MAUAJI YA HALAIKI.

Ujerumani sasa inayatambua mauaji ya watu wa jamii ya waherero kama mauaji ya halaiki.
Serikali ya ujerumani mjini Berlin sasa imeyatambua rasmi mauaji yaliyofanywa na nchi hiyo kipindi cha ukoloni katika koloni la ujerumani ya kusini-Magharibi ambayo ni Namibia ya sasa kama yalikua ni mauaji ya halaiki.

MBUNGE WA EAC APIGWA RISASI BURUNDI

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura.

UKWELI UNAUMIZA ILA UONGO UNAUA!

UKWELI UNAUMA NA KUUMIZA ILA UONGO NDIO UNAOUA.

Uoga ni zao la Uongo. Na ni mwaanzo wa kufilisika kiutu na ni angamizo la mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla. Hakuna sababu ya kuzuia imani yako kwa woga wako. Unachokiamini kutoka moyoni ni bora kuliko unachokionesha machoni au kukisema mdomoni.(Uoga ni kua unajiongopea hadi mwenyewe; Umekua muongo mpka unapokosa wa kumdamganya basi unajidanganya mwenyewe).

OBAMA AWAONDOA WASIWASI WAMAREKANI

Rais Barack Obama amewasihi Wamarekani kuacha kukata tamaa kutokana na wasiwasi wa kibaguzi uliojitokeza.

HABARI KUU MAGAZETINI SIKU YA LEO.

Soma kurasa za magazeti yako pendwa hapa…………>>>>https://t.co/rHyvDJjowP

Tuesday, 12 July 2016

DONALD TRUMP ALISHAWAHI KUMKUBALI HASIMU WAKE KUA RAISI WA NAREKANI

Binadamu tunaishi kwa kubadilika sana kulingana na mazingira. Mgombea wa uraisi nchini marekani alishawahi kumsifu hasimu wake wa sasa katika  kinyang'anyiro cha kiti cha uraisi kupitia chama cha Democrat, Hillary Clinton.

RONALDO AMFUNIKA MESSI KWA MAPATO KWA MWAKA 2015

Christiano Ronaldo ndiye mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes.

SANDERS NA CLINTON KUSIMAMA PAMOJA

Wagombea wawili wa chama cha Democrat nchini Marekani, Ben Sander na Hillary Clinton wanatarajiwa kuungana pamoja kwa kile kinachoonekana ni kujaribu kuunganisha nguvu ya chama chao dhidi ya Republican.

TOP 10 MUGABE'S HILARIOUS QUOTES ON RELATIONSHIP


Check out 10 Hilarious Quotes By President Robert Mugabe On Relationships.

MARAISI WA ZAMANI KUSUSIA KONGAMANO KUU LA CHAMA CHA REPUBLICAN

BUSH Snr na Jr, Mitt Romney Kutohudhuria kongamano la chama cha Republican litakalo fanyika mwezi huu.

MAKABURI YA WAFILISTI YAFUKULIWA ISRAEL

Ugunduzi uliofanywa na Israel unaweza kutatua dhana ya muda mrefu ya kwenye biblia kuhusu asili ya wafilisti.

SMARTWATCH YAKO INAWEZA KUWAPA WAHALIFU NAMBA YAKO YA SIRI YA ATM.

Smartwatch na vifaa vingne tunavyovivaa mwilini vinaweza kutoa namba yako ya siri ya ATM kwa wadukuzi "hackers".

Monday, 11 July 2016

UEFA YAMTAJA MCHEZAJI BORA WA EURO 2016

Leo jumatatu UEFA imemtaja mshambuliaji wa ufaransa na mfungaji bora wa mashindano hayo Antoine Griezmann kua ndiye mchezaji bora ya michuano ya ulaya kwa mwaka 2016.

SAMSUNG YAFELI JARIBIO LA KUKAA KWENYE MAJI

Simu ya kisasa ya Samsung Galaxy S7 inayopigiwa upatu kuwa na uwezo wa kustahimili kuwa chini ya maji imefeli majaribio ya shirika la moja la kutathmini ubora wa bidhaa za kielektroniki.
Programu ya simu hiyo ya Samsung Active ilizima punde baada ya kutumbukizwa ndani ya pipa la maji.
Kampuni hiyo ya kutathmini ubora wa bidhaa, Consumer Reports ilirejelea jaribio hilo kwa mara ya pili wakitumia simu tofauti na kama ile ya kwanza ikafeli.
Kampuni ya kutengeza simu hiyo ya Samsung ikijitetea imesema huenda simu hizo zilikuwa ni mbovu na hivyo kuruhusu maji kuingia ndani.
Simu hizo zilitumbukizwa ndani ya mapipa ya maji na kutolewa baada ya dakika.
Simu hizo za Samsung zilizima.
Kulikuwa hata na maji katika eneo la kamera za simu hizo mbali na viputo.
Kampuni inayotengeza simu hizo kutoka Korea Kusini Samsung imejitetea vikali ikisema kuwa Galaxy S7 Active, inayouzwa Marekani imefanyiwa majaribio kabambe na hata kupewa cheti maalum cha IP68.

GARI LIENDALO KWA KASI ZAIDI KUUNDWA NA LITATUMIA INJINI YA NDEGE.

Mradi wa kuunda gari liendalo kasi Zaidi duniani umefufuliwa na gari hilo linatarajiwa kujaribu kuvunja rekodi ya dunia mwaka ujao.

ETHIOPIA WAZIMA MITANDAO YA KIJAMII

Mitandao ya kijamii nchini Ethiopia imezimwa kwa sababu ya mtihani wa taifa. Waethiopia waliamka Wikiendi wakajipata hawana huduma hizo za mitandao kama Facebook, Twitter, Instagram na Viber.

KOREA KASKAZINI YATAKA MAWASILIANO NA MAREKANI

Maafisa wa runinga inayothibitiwa na serikali ya Korea Kaskazini, wanasema kuwa serikali ya nchi hiyo itakata mawasiliano na Marekani.

TOP 10 YA WACHEKESHAJI MAARUFU ZAIDI AFRIKA.

Wakati flani maisha yanaweza kwenda kombo lakini tunaweza kucheka tu. Hii hapa ni  Top 10 ya wachekeshaji maarufu zaidi Afrika.

MTOTO WA OSAMA AAPA KULIPIZA KISASI JUU YA KIFO CHA BABA YAKE.

Mwanaye wa aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda Osama bin Laden, ameapa kulipiza kisasi kwa mauaji ya babake.

URENO WATWAA UBINGWA WA EURO 2016 BILA CHRISTIANO RONALDO

Hatimaye timu ya taifa ya Ureno imetwaa kombe la mataifa ya Ulaya (EURO)2016 baadaya kuwazaba wenyeji wa mashindano hayo timu ya taifa ya Ufaransa goli 1-0.

Sunday, 10 July 2016

JE, HII NI SURA YA PILI YA KANALI MUAMMAR GADDAFI?

Imekua sio kawaida hata kidogo kwa aliyekua kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kuzungumziwa kwa upande hasi kwani kila mwafrika ukiacha wachache sana walikua na bado wanaamini Gaddafi alikua ni mpiganaji wa bara la Afrika.

WACHEZAJI SITA AZAM WATEMWA, WAWILI WAFELI MAJARIBIO

UONGOZI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, umetangaza rasmi kuwatema wachezaji sita kwa awamu ya kwanza huku nyota wawili wakifeli majaribio.

UTAMADUNI? MAMIA YA WATU KUPIGA PICHA ZA UTUPU

Mamia ya watu watavua nguo zao na kupigwa picha wakiwa tupu kusherehekea utamaduni katika mji wa Hull, Uingereza.

MNYIKA; SINA MPANGO WA KUHAMA CHADEMA.

Dar es Salaam. Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekanusha taarifa zinazodai kuwa anataka kuachana na chama hicho.

MWALIMU MKUU HUYU ANATUFAA SISI? (Sehemu ya 2)

HEADMASTER/MWALIMU MKUU
SEHEMU YA PILI.
Inaendelea ilipoiashia...

Saturday, 9 July 2016

FACEBOOK KUTUMIKA KUTUMA NA KUPOKEA PESA.

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni na hayawi hayawi sasa yamekua.

WATU 12 WAFARIKI KWENYE FOLENI

Watu 12 wamefariki nchini Indonesia kutokana na foleni ya magari iliyosababisha mamilioni ya watu kukwama barabarani siku kadha.

UNATAKA KUFUTA TAARIFA ZAKO KUTOKA GOOGLE? USIPITWE NA HII HAPA.

Ulishawahi kukaa ukafikiria kama unahitaji kufuta taarifa zako kutoka Google? Sasa usiwaze kila kitu ni kirahisi. Labda ulishawahi kutumia Google kutafuta taarifa flani na

Friday, 8 July 2016

KAMA UNAMILIKI SMARTPHONE NA UNAPENDA KU EDIT PICHA HAKIKISHA HAPITWI NA HII

Kama unamiliki smartphone au kompyuta na unapendelea kuhariri picha zako basi moja kati ya hizi application za kuhariri picha sio za kukosa!! Unaanzaje kukosa kwa mfano??

TOP 10 YA VIONGOZI WANAOTUMIA MAGARI YA BEI MBAYA KULIKO




Inaendelea.....

Haya magari ntatoa baadhi ya sifa zake kwa ufupi.

PILISI WANNE WAUWA NA SABA KUJERUHIWA

Maafisa wanne wa polisi mjini Dallas, Marekani wamepigwa risasi na kuuawa wakati wa maandamano ya kupinga mauaji ya watu weusi.

Thursday, 7 July 2016

ZIJUE NCHI AMBAZO VIONGOZI WAO WANATUMIA MAGARI YA BEI MBAYA KULIKO

Maisha ni kuchagua na kuchagua ni kupanga wenzetu walichagua. Wafalme, malkia, maraisi na masultani wanachagua wanachokitaka. Hapa nina orodha ya

MAREKEBISHO MADOGO KWENYE UTEUZI WA WAKURUGENZI WAPYA.

Taarifa iliyotolewa na ikulu hivi punde ni kua imefanya marekebisho kidogo kwenye uteuzi wa mkurugenzi wa manispaa ya Dodoma. Soma hapa>>http://lm.facebook.com/l.php?u=http%3A%2F%2Fmillardayo.com%2Fikulu54%2F&h=DAQEVAVqM&enc=AZOUxU6N-bqy1D41_Cj46xwFkxGijdqoPMrLC671vLcOeP2AKa745THKGyaXdUWfIOHLXyORPW8CRMptd1Xuy3nduL9A5T6LJ6HpSEcGpVyrs-tHvRD8RhmVvxaIBD2cOPGs-7_6r1HgxdbGIaRpG2dP60ED9bSnsU3sHDIiTF_FQBDs6fU_FChELx3R2mU-nPE&s=1

WAKURUGENZI WAPYA

Orodha ya wakurugenzi walioteuliwa leo na Rais Magufuli
Newsroom TZA

POLISI NCHINI MAREKANI WAMEMUUA MMAREKANI MWEUSI

Mtu mwingine mweusi amepigwa risasi na kuuawa mapema leo na polisi wa trafiki katika jimbo la Minnesota Marekani.

WACHEZAJI WANAPCHUKIWA ZAIDI DUNIANI KWA SASA

Mtandao wa Goal.com umetoa orodha ya wachezaji wanaochukiwa zaidi katika historia ya soka.

MANISPAA YA IRINGA YANG'ARA NG'ARING'ARI


Manispaa ya iringa imeibuka idedea kwenye swala la usafi kitaifa. Manispaa hio imeipiku manispaa ya moshi ambayo kwa kipindi kirefu imekua ikiongoza kwa usafi.

DONALD TRUMP AMSIFU SADDAM HUSSEIN



Wakati watu wengi wa marekani wakiamini kua Saddam Hussein alikua ni dikteta wa Iraq na mtu aliye fadhili ugaidi hali ni tofaututi kwa Trump.

MESSI KUTAKA RUFAA KUPINGA HUKUMU YA KESI YAKE

Wanasheria wa mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi pamoja na baba yake Jorge Messi wanatarajia kukata rufaa kupinga

Wednesday, 6 July 2016

NGUVU YA MJINGA HAIDHARAULIWI.

Usiidharau nguvu ya wajinga kwa maana wakiungana wana nguvu kubwa ya kuamua hata kama ni maamuzi ya kijinga.

ORODHA YA MABILIONEA WAKUBWA KWA MWAKA 2016 TANZANIA YUPO MMOJA TU.

Wakati tunaendelea kulalamikia ugumu wa maisha lakini upande mwngine hali ni tofauti. Ukweli n kwamba uchumi umekua mgumu kwa kila mtu, ila hii hapa ni orodha ya mabilionea wa Afrika mwaka 2016.

Mabilionea hawa wana utajiri wa pamoja unaofikia $80.94bilion ikiwa

RAISI OBAMA AMPIGIA "DEBE" WAZIRI WAKE WA ZAMANI.

Raisi wa marekani Barack Obama amefanya kampeni na aliyekua waziri wa mambo ya nje

MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA DAVID CAMERON WAANZA.

Conservative wapiga kura ya mrithi wa Cameron

Mchakato huo wa Kura unafanyika wakati ukiongezeka wasiwasi kuhusu taathira za kiuchumi baada ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya.

UNAJUA KUFANYA HAYA UKIWA NA SMARTPHONE YAKO? FANYA VINGI NA VIKUBWA UKIWA NA SMARTPHONE.

Unatumiaje "Simu janja" yako? Inawezekana ni mtumiaji mzuri wa smartphone lakini kuna "features" kwenye simu yako hukuwahi kujua kama zipo na labda pengine hufahamu kama simu yako inaweza kufanya jambo flani.

Kila mtu anajua jinsi ya
kutumia smartphone japo wengi wetu tumeanza kutumia smartphone bila kusoma "User Manual" na hivo kushindwa kuitumia simu hadi kiwango chake cha juu cha matumizi. Hivi ni baadhi ya ambavyo wengi hawajui jinsi ya kutumia.

1. UNA UWEZO WA KUPIGA PICHA 10 KWA SEKUNDE.ULISHAWAHI KUFANYA HIVI??  Ndio picha 10 ndan ya sekunde moja! Iko hivi kama wewe unatumia android fanya hivi;
Fungua camera yako > bonyeza kitufe cha "settings" kisha weka "Burst shot ON"(unaweza kutumia pia button ya kuongeza na kupunguza sauti)>> kisha kandamiza(gusa bila kuachia) "Shutter button" hadi utakapoona inatosha au hadi simu itakapofika idadi ya mwishi ya kuchukua izo "continuous pics". Nadhani umeelewa sasa unaweza kuchukua picha 100 nda ya sekunde 30 tu!! Jaribu sasa!!

2. UMECHOKA KUSOMA VITU VILIVYOPO KWENYE SIMU??

Usihofu fanya hivi....
Washa simu yako nenda kwenye "settings" kisha>> Accessibility na bonyeza "TalkBack". Kama hicho kitu hakipo kwenye simu yako nenda kakipakue Play store. Baada ya hapo rudisha simu yako kwenye home screen na simu itasoma chochote utakachokibonyeza pamoja na taarifa zinazoingia. Ili kuweza "Ku swipe" simu yako tumia vidole viwili badala ya kimoja.
Kama hupendi jinsi simu inavyoongea unaweza kubadili sautu na speed kwa kwenda kwenye "Settings" >>>Accessibility >>>text-to-speed options na badili sauti na speed. Na kisha nenda kwenye "Settings" na uweke "Hands-free mode" ili simu iweze kutambua anaekupigia na kukutumia ujumbe.

3. KU BLOCK TEXT NA SIMU YA MTU AMBAE HUTAKI AKUPIGIE AU AKUTUMIE UJUMBE.

Nenda kwenye "Settings" >>>Call settings >>>chagua Incoming calls na bonyeza call block list >>>create. Apo utaingiza namba ya mtu unaetaka asikupate, kama huna kichwani bonyeza kwenye alama ya picha unayoiona kwenye screen yako kisha itakupeleka kwenye phone book au call history na uko utachagua namba ya muhusika.
Ila unaweza kumtoa mtu kwenye kifungo hiki.

Nadhani umeongeza maarifa juu ya kutumia smartphone yako na kama unakitu hukielewi unaweza kuacha comment yako hapo chini au kwenye ukurasa wa facebook. Tukutane wakati mwingine bye byee!!!

Tuesday, 5 July 2016

FBI WATOA TAARIFA YAO YA UCHUNGUZI DHIDI YA HILLARY CLINTON

HILLARY CLINTON KAKALIA KUTI KAVU??

FBI wametoa taarifa yao ya uchunguzi juu ya tuhuma zinazo mkabili mgombea wa wa uraisi wa marekani kupitia chama cha Democrat,

DONALD TRUMP NA MAREKANI MPYA(Muendelezo)

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya marekani(muendelezo...)

KWA MARA YA KWANZA KABISA SAYARI YA JUPITER (ZOHALI) KUFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA.

NASA imetoa taarifa kua chombo chao cha JUNO kilichotumwa mwaka 2011 kewasili mapema leo asubuh na kuanza kazi yake ya kuizunguka sayari hio. NASA  wanatarajia kukitumia chombo hicho hadi mwezi February 2018. Kwa maelezo zaidi soma hapa..>>>http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/07/160704_juno_spacecraft

TUIGE MFANO WA ETHIOPIA.

Licha ya changamoto za ukame zinazo ikumba Ethiopia lakini bado wana nia ya dhati ya kuifanya Ethiopia kua taifa  na lenye nguvu kiuchumi barani Afrika.

Taifa lolote ambalo lina watu makini, viongozi wenye mawazo ya mbali, waadilifu na waliojitoa huweza kuendelea kwa haraka zaidi kuliko inavodhaniwa.

RAISI MAGUFULI ATENGUA NA KUTEUA WENGINE.

Raisi magufuli afanya mabadiliko kwenye benki ya TIB

Taarifa niliyoipokea kutokea ikulu inasema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 48 cha sheria ya tafsiri za sheria

MABAKI YA NDEGE YA MALAYSIA KUCHUNGUZWA DAR.

Ndege iliyopotea Malaysia kuchunguzwa nchini


Florence Majani
Bawa mojawapo la ndege hiyo linadaiwa kupatikana hivi karibuni katika Kisiwa cha Kojani,

DONALD TRUMP NA MAREKAMI MPYA.

Donald Trump. Mambo makubwa yanayoibeba imani yake juu ya Marekani.

1. Wamarekami wengi wenye asili ya kiarabu walishangilia lile shambulizi la september 11 2001. Hili ni shambulio baya kabisa kwa nchi ya marekani miongo kadhaa.

2. Anaamin kua miskiti yote nchin marekani inapaswa

PANYA WA SUA KUPIMA WAGONJWA WA KIFUA KIKUU ETHIOPIA.

Panya wa Sokoine kutumiwa Ethiopia

Wanasayansi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine nchini Tanzania wanapanga

Monday, 4 July 2016

NATO na Urusi "Kupooza" Mvutano.

NATO na Urusi kufanya mazungumzo ya pamoja baada ya kilele cha mazoezi ya kijeshi huko Warsaw.

NATO and Urusi watafanya mazungumzo rasmi mara  baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kijeshi mjini Warsaw wiki hii.

NI JEURI YA PESA AU KIBURI??

Klabu ya Manchester united ya uingereza imesisitiza kua inataka kumsajili tena kiungo wa ufaransa na

DHIMA YA KITABU CHA REPUBLIC (2)

#REPUBLIC_SEHEMU_YA_2

Baada ya kukubaliana maana hak na katba Socrates aliamua kueleza kuhusu katba isiyo hak. Lakin anaanza kwanza kutueleza n vp mtawala "philosopher king"

HASIRA ZAONGEZEKA MIONGONI MWA WAKAZI WA BAGHDAD.

Kufuatia shambulio la kigaidi la lililotekelezwa na kikundi cha ISIL na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200 wengi wao wakiwa n watoto kimeamsha hasira miongoni mwa wakazi wa Baghdad wengi wao wakiilaumu serikali ya Iraq kushindwa kuwalinda.
Shambulio hilo la mapema jumapili limesababisha tafrani kubwa miongoni mwa wananchi wa Baghdad kwa kua licha ya  serikali kutangaza kuukomboa mji wa fallujah ambao ulikua n ngome muhimu kwa ISIL  lakini bado haijaweza kuhakisha kua maeneo yote ya Iraq yanapata ulinzi wa kutosha ili kukabiliana na wanamgambo wa ISIL.

RETHINK and then REWRITE

Ukiisoma hii article ni kama unamsikiliza mwanamapinduzi wa kiafrika!! https://www.africanexponent.com/post/history-of-europeans-in-africa-is-not-african-history-3231

UINGEREZA KUPUNGUZA KODI KWA MAKAMPUNI.

Uingereza kuvutia makampuni ya biashara

Waziri wa fedha wa Uingereza George Osborne ameeleza mipango ya wizara yake yenye lengo la kupunguza kodi muhimu ya faida katika biashara.
Hatua ya Osborne ni sehemu ya mkakati wa kiuchumi katika harakati za kuvutia uwekezaji mpya, na hii inafuatia kura ya maoni iliyopigwa mwezi uliopita ambayo iliamua Uingereza isite kuwa mwanachama wa umoja wa ulaya.
Osborne aliliambia gazeti la Financial Times kwamba anataka kupunguza kodi ya shirikishi kutoka asilimia ishirini hadi chini ya asilimia kumi na tano.mwandishi wa BBC wa masuala ya biashara ameeleza kwamba kura ya maoni ilikuwa ni mkakati wa kuisaidia Uingereza kuvutia uwekezaji kutoka kwa kampuni mbali mbali mpango ambao inawezekana haukufanikiwa kufuatia kura hiyo ya maoni.

UNADHANI TATIZO LA AJIRA NI LAKO PEKEE?

Kuna msemo husema kua "kukimbia tatizo sio njia ya kulitatua". Huyu jamaa alikimbia kwao na kwenda kusaka kazi CHINA na hii ni story alotuletea.
https://m.facebook.com/l.php?u=https%3A%2F%2Fwww.africanexponent.com%2Fpost%2F7480-is-the-grass-greener-on-the-other-side-of-the-fence&h=6AQEihDi2&enc=AZPfcmQcb3iBfAxSuYjDfJr2aabJTy-LyTeVnCPZGNDpytp3OuRDUXNcsaoQ-gO03tU69DwuBSHfxh8BJ39pRv525qGKjc5fe5S-vvu1RXj3cxQEvBD9rhdcQk5FdHzTkvL4NrqsU0R6vX1Oo4ERZouVtKPvyXhFwCrhb8ptPvcgh-1BQC9wHULFyuUwX4v-h2I&s=1

TAZAMA MIMEA HII NA UTAJIFUNZA KUA KATIKA MAISHA HAKUNA KUKATA TAMAA.

Inawezekana unaona maisha ni magumu saana na huna budi kukata tamaa. Lakini kila siku amini kua neno "Nimeshindwa au Siwezi" halipo katika dunia yako.

Tazama picha hizi kumi ambazo zinakuonesha kua kuna uwezekano wa maisha "kutokeza" popote utakapoamua kutokea. 

https://www.africanexponent.com/post/7478-10-plants-which-conquered-death

MAUDHUI YA JUMLA YA KITABU CHA REPUBLIC [PLATO]

WAKATI FLANI NI VEMA TUJIHUKUMU WENYEWE NA BAADA YA HUKUMU TUJIADHIBU KWANZA KABLA HATUJAADHIBIWA. KATIKA MAISHA KUKOSEA KUPO LAKINI NAFAS YA KUJISAHIHISHA PIA IPO PALE PALE.  UONGOZI NI MAISHA YA MAKOSA LAKIN LAZMA TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA YETU. HUWEZI KUA BORA PASIPO KUKOSEA. 

#REPUBLIC ni moja kati ya vitabu maaruf saana duniani. Kiliandikwa na Mwanafalsafa nguli #PLATO yapata takriban karne 4K.K (Kabla ya Kristo). Kitabu kimeshehen mazingumzo ya wanafalsafa nguli akiwemo #Socrates ambae pia ni mwalim wa #Plato. Kitabu hiki kinaeleza maana ya HAKI, utawala wa hak na hak ya mtu. watu weng wakiongozwa na Socrates waltoa maana ya hak kua n kutoa kile unachodaiwa,

FALSAFA YAKO NDIO INAKUONYESHA WEWE UKO VIPI NDANI

Falsafa ya "TOTAL FOOTBAL"


MCHEZO HUU HAUHITAJI HASIRA WALA UBABE. 

Unajua huwa napenda sana jins ambavyo FC Barcelona hua inacheza. Mfumo huu uliàasisiwa huko Uholanzi na mfumo huu uliletwa na Johan Cruyff pale FCB(yeye alikua akiutumia kwenye team yake ya Ajax na ile ya taifa). Katika mfumo huu kila mchezaji anapaswa kuchangia katika upatikanaji wa goli na unaruhusu mchezaji mwingne kuchukua nafasi yà mwenzake mkiwa mchezon.

JOINING INSTRUCTIONS

PAKUA HAPA FORM ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO MWAKA 2016 KWA SHULE ZOTE.

http://www.tamisemi.go.tz/noticeboard/joining-instructions

ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2016

Ofisi ya Rais TAMISEMI imetoa orodha majina ya kidato cha tano 2016

http://tamisemi.go.tz/form_five_selection/

MWALIMU HUYU ATSTUFAA SISI WANAFUNZI?

Kaspersky: *SHULE SERIES* *HEAD MASTER/ MWALIMU MKUU* *SEHEMU YA KWANZA* Nakumbuka kwa uzuri kabisa kua siku hio ilikua n nzuri saana, maama niliamka asubuhi na mapema nkavaa sare zang mpyaaa za shule yetu, nilibeba mfuko wangu wa madaftar...na safar ikaiva kwenda kuanza shule rasmi! Nilipofika shule nilipokelewa kwa tabasamu za walimu na wanafunzi pale shuleni. Kila mtu alifurahi kwa kua mda mfupi ndipo shule yetu ilikua imeanzishwa kwa juhudi za mkuu wa shule bwana Rev.Democrat. Kwa kweli mkuu wetu alipendwa saana kutokana na juhud zake za kuipigania shule kwa maslah ya watoto pale kijijin na vijiji vingne vya jirani. Lakin sio km watu wote walikubaliana nae la! Wengne walimpinga. Kutokana na uchanga wa shule tulisoma kiugumu ugumu ila mkuu mara zote alisisitiza kuthubutu, kujiamin na kujitegemea. Kwa kweli ndoto yake ilikua n kuleta usawa na maendeleo kwa kila mtu lakin haikua kaz rahis, alifanikiwa kwa kias chake lakin sio km alivyoota kua ije kua. Miaka ilipita shule isonga mbele japo changamoto zilikua nying mwalim mkuu alijarbu kuzitatua kwa kutumia *akili, busara, utashi, weled na maarifa*. Alihimiza kujitoa kwaajili ya wengi. Nakumbuka siku moja alitukusanya wanafunzi na wazaz/walez akisema kuna jambo alitaka kutuambia.😥😢 Tulifika kwa wingi na kama ilivo ada tulikua na furaha ila baada ya muda mfup hapakua na furaha hata kidogo😢😥, nakumbuka tulikua tumejiinamia hakuna mtu aloweza hata kunong'ona ndipo nilisikia sauti kutoka mbaaal zikijisifia kua *"Tumeshinda! Tumesjinda"* zikiambatana na vicheko vya kejeli. Mwalim mkuu alituambia kua hawez kuendelea kuiongoza shule yetu. Hiki ndicho kilileta huzuni😥. Ningali najiuliza saana juu ya zile sauti na vicheko ni za akina nani? 😳 **~~~** Siku zilienda mwishowe tukampata *Mwalimu mkuu Mpya* huyu mkuu hakua km yule mwanzo😥🤔 aliamuru shule yetu iandikishe mtoto yeyote bila kujali atokapo. Nakumbuka siku moja tulikua darasani tukiwa tumejazana saana kwa bahat mbaya mwanafunzi mmoja akajamba! Hali ya hewa ibadilika ikawa mbaya mno tukasukumana na kupiga kelele labda kila mtu avute hewa ya *Oksijeni* japo mara moja😢🤔. Mwalimu mkuu baada ya kuona vile akaamuru tufungue madirisha. Kwa kua darasa letu lilikua ule upande wa choo cha wanafunzi basi *NZI* walimiminika darasan na tuliposema *"Jaman fungeni madirisha!"* mkuu akasema *"Msifunge madirisha kwan nzi wakiingilia upande huu wa kulia watatokea kushoto"*. Niliguna kwa sauti mkuu akageuka na kuniambia *"Nimefanya hivi ili tupate kupumua, tumia mkono na daftar lako kufukuza nzi ila hatutafunga madirisha"*😥😳 Namkumbuka mwali huyu km Mr.FreeAir. Hakukaa muda sana akaja mwingne... (Bado nipo shule) *Itaendelea....*